Saturday, May 20, 2017

Wananchi wamtimua Ofisa Mtendaji wa Kijiji



Wananchi wa Kijiji cha Embaseni iliyoko wilayani Arumeru mkoani Arusha wamesema kuwa hawamtaki ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Glory Urio kwa madai ya kupinga utekelezaji wa maendeleo ya kijiji chao.
Glory alitolewa malalamiko hayo leo kwenye mkutano wa wananchi wote wa kijiji waliokuwa wanajadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika eneo hilo viwanja vya Embaseni
Katika majadiliano hayo ndiko kukaibuka hoja ya kumtaa ofisa mtendaji huyo, kwa madai ya kupinga kila utekelezaji wa mambo ya maendeleo yanayopangwa na wananchi hao ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati, madarasa ya shule sambamba na miundo mbinu ya maji
Anande Nanyaro amesema kuwa awali waliamua kwa pamoja kupitia kwenye mkutano wa kijiji kujenga zahanati ya karibu kufuatia umbali mrefu wanayotembea kufuata huduma ya afya katika hospitali ya Tengeru lakini zoezi hilo limekwama kwa mda mrefu mbali na kuchangishana fedha
Vitalis Massawe amesema kuwa anaiomba serikali kumtafutia sehemu nyingine pa kumuhamishia mtumishi huyo kwa madai amekwisha kuchelewesha mambo mengi huku matatizo yakizidi kuwaandama
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha embaseni Gadiel Mwanda amesema kuwa wananchi hao wamechanga kiasi cha Sh 10 milioni kwa ajili ya ujenzi wa zahanati kufuatia changamoto ya umbali wa kituo wanachotumia cha tengeru, lakini zoezi hilo limekwamishwa na itikadi za kisiasa
Akijibu hoja hizo Urio amesema kuwa hajakwamisha ujenzi huo bali wananchi hao wanashindwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za ujenzi wa zahanati hiyo sambamba na uibuaji na utekelezaji na uendelezaji wa miradi

0 Responses to “Wananchi wamtimua Ofisa Mtendaji wa Kijiji ”

Post a Comment

More to Read