Monday, May 22, 2017
Kauli ya TFF baada ya ajali ya Ruvu Shooting hii Leo
Do you like this story?
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko taarifa za
kupata ajali kwa msafara wa timu ya Ruvu Shooting FC iliyotokea leo
barabara ya Manyoni mkoani Singida wakati kikosi hicho kikitokea
Shinyanga kwenda Pwani.
Taarifa
kutoka Singida zinasema gari hilo lilipata ajali baada ya kupasuka
tairi moja la mbele hivyo kuyumba na kuacha njia eneo la Itigi -
kilometa 200 kutoka Singida mjini kuelekea Manyoni hivyo kutoka
barabarani kuu kabla ya kugonga mti.
Taarifa
hizo zilizothibitishwa na Masau Bwire, zinasema wachezaji watatu
akiwamo Bwire mwenyewe ndio waliopata majeraha na kukimbizwa Hospitali
ya Mkoa wa Singida kwenda kutibiwa. Wachezaji hao ni Yussuf Nguya, Abdul
Mpambika na Saidi Dilunga.
Timu
hiyo ilikuwa mkoani Shinyanga ilipocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya
Vodacom msimu wa 2016/17 dhidi ya Stand United na kupoteza kwa mabao
2-1, hata hivyo imebaki kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao baada ya
kushika nafasi ya saba.
Mara
baada ya kupata taarifa hizo, Rais wa TFF Jamal Malinzi mara moja
ametuma salamu za kuwapa pole uongozi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania pamoja na timu nzima ya Ruvu Shooting.
“Nawapa
pole viongozi wote, makocha na wachezaji. Na kwa wachezaji ambao
wamejeruhiwa na viongozi wote waliojeruhiwa akiwamo ndugu yetu Masau
Bwire, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka,” amesema Malinzi.
Rais
Malinzi alimshukuru Mungu kwa kuepusha vifo kwa wanafamilia hao wa
mpira wa miguu hasa wakati huu Watanzania wakiwa makini kufuatilia
maendeleo ya timu za taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)