Monday, May 22, 2017
Kauli ya Waziri Mwigulu Nchemba toka Kibiti
Do you like this story?
Serikali
imerejea kauli yake ya kuhakikisha watu wanaofanya mauaji ya polisi
na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika wilaya za Kibiti na Rufiji
Mkoani Pwani wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa operesheni
maalum inayoendelea katika wilaya hizo ni lazima itoe matokeo
yatakayomhakikishia kila mwananchi maisha salama ndani ya nchi hii.
Ametoa
kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua kambi maalum ya
operesheni ya kuwatafuta wauaji wa baadhi ya viongozi wa chama cha
mapinduzi wilayani Kibiti, akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkoani Pwani ambaye pia ni mkuu wa Mkoa huo Mhandisi
Evarist Ndikilo.
Katika
maelezo yake, Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema hisia zilizokuwepo
kwamba pengine mauaji hayo yanahusishwa na katazo la biashara ya mazao
ya misitu ukiwemo mkaa, misimamo ya kidini, Ujambazi ama ugaidi siyo za
kweli, bali ni mchezo uliobuniwa na kundi la watu kwa sababu ambazo
haziko wazi na kwa hiyo ni lazima vitendo hivyo vikomeshwe mara moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)