Monday, May 22, 2017
Ufafanuzi kuhusu soda ya Novida kuwa na Virusi vya Ebola
Do you like this story?
Mamlaka
ya Chakula na madawa (TFDA) imewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo
zimekuwa zikisambazwa kwa nyakati tofauti kwenye mitandao ya kijamii
kuwa kuna soda aina ya ‘Novida’ kutoka nchini Nigeria zimeingizwa nchini
kinyemela na zina sumu ya virusi vya Ebola na tayari zimesababisha vifo
vya watu 180 nchini humo.
Taarifa
ya Mamlaka hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni
mwendelezo wa taarifa yake ya awali iliyotolewa mwezi Aprili 2017
inabainisha kuwa taarifa zinazosambazwa za kuingizwa soda zenye sumu ya
Ebola haina ukweli na inapaswa kupuuzwa.
Kwenye
taarifa hiyo, TFDA imeeleza kuwa inatambua uwepo wa soda ziitwazo
Schweppes Novida zinazozalishwa na viwanda vya Coca-Cola Kwanza,Bonite
na Nyanza Bottlers na soda hizo zinazalishwa kwa kuzingatia mifumo bora
ya uzalishaji na zinakidhi vigezo vya usalama na ubora.
‘’Kama
ilivyo kwa bidhaa nyingize za chakula,vipodozi,vifaa vya tiba na
vitendashi,soda za Schweppes Novida ambazo zimesajiliwa na TFDA
zimekuwa zikifuatiliwa katika soko kupitia mifumo liyopo ya udhibiti ili
kujiridhisha kuwa zinaendelea kukidhi vigezo vya usalama na ubora kwa
lengo la kulinda afya ya mlaji’’inabainisha sehemu ya taarifa ya TFDA .
Soda
aina ya Schweppes Novida kwa hapa nchini ilizinduliwa mwaka 2013,
inatengenezwa na kusambazwa na viwanda vya Coca-Cola vilivyopo katika
mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro.Soda hizi
zinazopendwa na wateja zinatengenezwa kwa ujazo wa ml 300 na ml 500 zipo
za aina ya Mandarin Cooler zenye ladha murua ya machenza na Pineapple
Breeze zenye ladha ya Nanasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)