Thursday, June 8, 2017
NDESAMBURO AMUIBUA DR SLAA
Do you like this story?
Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa
amesema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha Mzee Philemon Ndesamburo na kueleza
jinsi walivyokijenga chama pamoja.
Dk.
Slaa amesema kuwa licha ya Ndesamburo kuwa na utajiri mkubwa, lakini hakuuona
kuwa ni kitu bali ni nyenzo ya kuwakomboa wananchi katika sekta mbalimbali.
Dk.
Slaa ameitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu aliyekuwa Mbunge wa Moshi
Mjini kwa miaka 15, Mzee Philemon Ndesamburo alipozikwa nyumbani kwake KDC
Moshi baada ya kufariki wiki iliyopita alivyopata matatizo ghafla akiwa ofisini
kwake.
Dk.
Slaa ambaye sasa anaishi Toroto nchini Canada baada ya kujiuzulu wadhifa
wake na kuachana na siasa tangu mwaka juzi, alisema kuwa ameshtushwa sana na
kifo cha ghafla cha kiongozi huyo tegemeo. Alieleza kuwa licha ya wao kubaki na
majonzi, lakini anaamini kazi ya Mungu haina makosa wala haihojiwa.
"Ni
kweli nimefanya kazi na Ndesamburo, tumejenga CHADEMA kwa pamoja hasa kipindi
cha mwaka 2003 hadi 2005 ambapo tulizunguka nchi nzima," alisema Dk. Slaa
na kuongeza kuwa licha ya mazingira magumu waliyokutana naye kwenye harakati za
kukitangaza chama hicho, Mzee Ndesamburo hakulalamika alipotakiwa kulala chini,
lakini aliona hizo ni changamoto za kutafuta ukombozi.
Aidha,
Dk. Slaa alisema kuwa Mzee Ndesamburo alikuwa msikivu na mwenye kuelewa na kuwa
tayari kuwasaidia wengi kwa hali na mali kwani mara kadhaa alitoa mali zake
kuwasaidia wagombea wa CHADEMA na hata yeye mwenyewe kwenda kuwapigia kampeni
bila kujali umbali aliotakiwa kwenda.
Akizungumzia
kifo chake, Dk. Slaa alisema kuwa kifo hicho ni cha kusikitisha kwa sababu
alifariki ghafla, hakupata nafasi ya kuagana na ndugu jamaa na marafiki.
"Wakati
mwingine afadhai mtu akiugua mnajiandaa kisaikolojia, ila akifariki ghafla tu,
huwa ni kazi ngumu kuipokea ile hali.Kazi kubwa iliyobaki kwa watanzania sasa
ni kutekeleza yale yote ambayo Mzee Ndesamburo amewaachia huku tukimuombea
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi."
Dk.
Slaa aliondoka nchini mwaka 2015 baada ya kujiuzulu wadhifa wake kufuatia chama
chake kumpokea na kumpa nafasi ya kugombea urais, aliyekuwa kada nguli wa CCM,
Edward Lowassa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NDESAMBURO AMUIBUA DR SLAA”
Post a Comment