Thursday, June 8, 2017
SABABU YA MECHI YA TAIFA STARS Vs LESOTHO KUPIGWA CHAMANZI BADARA YA UWANJA WA TAIFA
Do you like this story?
MCHEZO wa
kwanza wa Kundi la kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya
wenyeji, Tanzania ‘Taifa Stars’ na Lesotho ‘Mamba’ utachezwa kwenye Uwanja wa
Azam Complex, hamazi, Dar es Salaam Jumamosi kuanzia Saa 2:00 usiku.
Hayo
yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
Malinzi
amesema sababu za mchezo huo kufanyika Uwanja wa klabu ya Azam ni kutokana na
Uwanja wa Taifa kuwa katika matengenezo madogo.
Rais
Malinzi amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Azam Complex,
kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri.
Taifa
Stars itaingiaa kwenye mchezo huo ikitoka kwenye kambi ya wiki moja mjini
Alexandria, Misri.
Nahodha
Mbwana Ally Samatta hakuwepo Misri na anatarajiwa kuungana na wenzake hapa Dar
es Salaam akitokea Ubelgiji ambako anachezea klabu ya KRC Genk.
Kiungo wa
DC Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa AFC Eskilstuna ya
Denmark, Thomas Ulimwengu wao walikuwepo Misri na wako tayari kwa mchezo wa
keshokutwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SABABU YA MECHI YA TAIFA STARS Vs LESOTHO KUPIGWA CHAMANZI BADARA YA UWANJA WA TAIFA”
Post a Comment