Sunday, August 27, 2017
DARASA LA SABA WAMZUIA LEMA KUFANYA MIKUTANO JIMBO KWAKE
Do you like this story?
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) amezuiwa kufanya mikutano ya hadhara jimboni kwake kati ya
leo (Agosti 27, 2017) hadi Septemba 8, 2017 ili kupisha shughuli mbili
zinazotakiwa kufanyika mkoani humo.
Katika barua iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, na
kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo imeeleza
kuwa ombi la mbunge huyo la kutaka kufanya mikutano limezuiwa, kwanza kwa
sababu ya maandalizi ya mitihani ya darasa la saba lakini pili, maandalizi ya
ujio wa mwenge wa uhuru.
Zuio hilo lilinukuu barua ya tarehe 23/8/2017 ya mbunge hiyo
iliyokuwa ikitoa taarifa za mkutano wa hadhara.
“Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha
inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yenye ratiba ya 27/8/2017 hadi 1/9/2017
kwa sababu zifuatazo;”
“Maandalizi ya kuhitimisha mitihani ya darasa
la saba na mwenge wa uhuru ambayo ni matukio makubwa ya kitaifa kwa tarehe
hizo. Baadhi ya viwanja vilivyopo kwenye ratiba yako ya mikutano navyo vipo
kwenye maandalizi kwa ajili ya moja wapo ya matukio hayo.”
Aidha, Polisi wamemueleza mbunge huyo kuwa, kutokana na sababu
hizo anaweza kupanga mkutano muda wowote baada ya kumalizika kwa mitihani ya
darasa la saba yaani Septemba 8.
Kamanda wa Polisi alisema pia, Polisi wanahitajika katika
maaandalizi ya mwenge na mitihani hiyo, hivyo hawawezi kupata Polisi wa kutosha
kugawanywa sehemu zote hizo tatu.
Kwa upande wake, Lema amepinga sababu zote zilizotolewa na Polisi
na kusema kuzuiwa kwa mikutano yake ni njama za kisiasa kwani kwenye mikutano
10 aliyofanya imekuwa ya mafanikio makubwa, wananchi wamemuunga mkono na pia
wamepata nafasi ya kufahamu ukweli wa mambo mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ DARASA LA SABA WAMZUIA LEMA KUFANYA MIKUTANO JIMBO KWAKE”
Post a Comment