Sunday, August 27, 2017

MAMBO SITA YANAYOTOKEA SASA BILIONEA BILL GATES ALIYATABIRI MWAKA 1999




Bill Gates ni bilionea namba moja duniani. Utajiri wake ameupatia kwenye sekta ya teknolojia kwakuwa muanzilishi-mwenza wa kampuni ya Microsoft. Kwa kipindi chake, kuweza kuanzisha kampuni ya maswala ya teknolojia tu ilikuwa yahitaji uwezo mkubwa wa kuangalia uelekeo wa dunia na kuweza kuendana nao. Kana kwamba hiyo haitoshi, kudhihirisha uwezo wake huo – aliandika mambo kadhaa kwenye kitabu chake cha mwaka 1999 – mambo ambayo yote yamekuwa kweli sasa hivi.

 Katika kitabu hicho, “Business @ the Speed of Thought,” Gates alitabiri mambo sita ya muhimu sana ambayo yangetokea kwa miaka michache inayofata kutokana na maendeleo ya teknolojia. Haya ni mambo sita aliyotabiri ambayo kwa sasa yamekuwa kweli:

Mchakato wa ajira kufanyika kupitia mtandao
aliandika kwamba: watu watakuwa wanatafutafursa za ajira kwa njia ya mtandao. Leo hii kuna tovuti nyingi sana maarufu kwa ajili ya kuunganisha watu kwenye soko la ajira. Moja ya tovuti hizo ni LinkedIn ambapo mtu anaweza kufungua akaunti yake na kuweka taarifa kadhaa kama historia yake ya elimu, sehemu alizowahi kufanya kazi, muda aliofanya kazi hiyo, watu wanaoweza kuthibitisha kuwa wanamjua kw akufanya naye kazi. Pia, muajiri anaweza kuingia na kuangalia watu watakaoweza kufaa kwenye nafasi ya kazi iliyo wazi bila hata kuhitajika kumuita waonane.

Vipindi vya televisheni kuunganishwa kwenye tovuti na kuangaliwa kupitia mtandao
Aliandika kwenye kitabu hicho kwamba, “Viungio (link) zinazotokea kwenye televisheni wakati kipindi kinaendelea zitasaidia sana vipindi vya televisheni kuweza kuangaliwa na watu wengi hata kama hawapo kwenye televisheni hizo.”

Kwa sasa tunaona hata hapa kwetu kwamba kwenye vipindi vingi wanaweka viungio vinavyoweza kumfanya mtu aweze kufatilia matangazo hayo kwa njia ya mtandao kama kwa matumizi ya “hashtag,” majina ya akaunti zinazotumika kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Instagram ili wasioweza kuangalia televisheni waweze kufatilia matangazo hayo kwa kutumia mitandao kupitia simu zao za viganjani.
Matangazo/kujitangaza kisasa zaidi

Aliandika kwamba, “vifaa tunavyotumia (simu, kompyuta, tablet, n.k) vitakuwa vitawezeshwa kujua tabia yako ya manunuzi, hivyo kukurahisishia machaguo kwa kukuletea vitu unavyopenda utakapojaribu mara nyingine.”

Sasa tunaona kwamba unapotembelea tovuti nyingi, matangazo yanayotokea yanatokana na historia yako ya manunuzi uliyofanya au historia ya vitu ulivyowahi kutafuta kabla.

Kushika kasi kwa mitandao ya kijamii
Aliandika kwamba, “tovuti binafsi zitaanzishwa zitazowawezesha watu kuweka taarifa zao kwa ajili ya wanafamilia na marafiki zao, na litakuwa jambo la kawaida sana.”

Leo hii mitandao ya kijamii kama Twitter ina mamia ya mamilioni ya watumiaji, huku tukishuhudia mtandao namba moja, Facebook, ukiripoti kuwa na watumiaji zaidi ya bilioni mbili.

Wasaidizi binafsi
Gates aliandika kwamba teknolojia itasaidia “kuunganisha vifaa vyote kwa njia ya kisasa zaidi.” Ushahidi wa hili ni pale unapotumia Google au Amazon Echo zinazomrahisishia mtumiaji kufanya shughuli mbalimbali.

Vifaa vya kisasa vinavyobebeka kirahisi
Kwenye kitabu chake, Gates aliandika kwamba, tofauti na sasa, “watu watakuwa wanatumia vifaa vidogo zaidi ambavyo wanaweza kuwa navyo wakati wowote kwenye matembezi yao na vyenye uwezo wa hali ya juu wa kuwawezesha kufanya lolote watakaloamua”

Kwa miaka kadhaa sasa tumeshuhudia maendeleo ya haraka kwenye sekta ya kiteknolojia hasa simu za kiganjani, tablet na kompyuta mpakato (laptop) ambapo watengenezaji wa vifaa hivyo wanazidi kuvifanya kuwa vyepesi na vinavyobebeka kirahisi ili mtumiaji aweze kwenda navyo sehemu yoyote.

0 Responses to “ MAMBO SITA YANAYOTOKEA SASA BILIONEA BILL GATES ALIYATABIRI MWAKA 1999”

Post a Comment

More to Read