Wednesday, September 13, 2017

Lady Jay Dee amvuta tena Justin Campos



 
 Msanii Lady Jay Dee amvuta tena kwa mara nyingine muongozaji wa video kutoka nchini Afrika ya kusini ‘Justin Campos’ katika nyimbo yake mpya ya ‘I Miss You’ ambaye ndio ameifanya video ya wimbo huo.
Lady jay Dee ameeleza kuwa video yake ya nyimbo ya I Miss You imefanywa nchini Afrika ya Kusini na mtayarishaji akiwa ni Justin Campos ambaye ndiye aliefanya video yake ya nyimbo iliyofanya vizuri ‘Ndi ndi ndi’ nyimbo ambayo mpaka sasa inajumla ya watazamaji  zaidi ya milioni 1 katika mtandao wa YouTube.
‘’Video ya nyimbo yangu mpya I Miss You itatoka Ijumaa hii na video imeongozwa na mtayarishaji Justin Campos kutoka nchini Afrika Kusini ambaye ndio alie fanya video yangu ya Ndi ndi ndi’’ amesema Lady Jay Dee.
Nyimbo ya I Miss You ndio kazi ya kwanza kwa msanii Lady Jay Dee tangu alipotoa Album yake ya Saba ‘Women’ album iliyotoka mwaka huu.

0 Responses to “Lady Jay Dee amvuta tena Justin Campos”

Post a Comment

More to Read