Tuesday, September 12, 2017
Liverpool wapinga kadi nyekundu ya Sadio Mane
Do you like this story?
Majogoo wa jiji Liverpool, wamekata rufaa ya kupinga adhabu
ya mshambuliaji wao kutoka nchini Senegal Sadio Mane, baada ya kuonyesha
kadi nyekundu wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Man
City, uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.
Mane alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kupiga teke mlinda mlango wa
Man City Ederson sehemu za usoni na kumsababishia maumivu makali, ambayo
yalimzuia kuendelea na mchezo huo, uliomalizika kwa majogoo wa jiji
kufungwa mabao matano kwa sifuri.
Mshambuliaji huyo ambaye ni msaada mkubwa kwa Liverpool, alimuomba
radhi Ederson kwa rafu mbaya aliyomchezea, kupitia mtandao wa kijamii wa
Facebook mara baada ya mchezo kumalizika katika uwanja wa Etihad huko
mjini Manchester.
Mane aliandika: “Ninatarajia na kumtakia Ederson kupona kwa haraka.
“Niuwie radhi kwa kukuumiza sehemu za usoni, halikua kusudio langu
kufanya vile, ila ilitokea kutokana na mazingira yaliyokuwepo kati yetu
wakati tukiwania mpira. Ninarudia tena kwa kukutaka msahama na
ninatarajia kukuona tena uwanjani siku za karibuni.”
Chama cha soka nchini England FA kinatarajia kusikiliza rufaa ya Liverpool hapo kesho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Liverpool wapinga kadi nyekundu ya Sadio Mane”
Post a Comment