Tuesday, September 12, 2017
Wilshere, Sanchez kuanza dhidi ya FC Cologne
Do you like this story?
Kiungo Jack Wilshere na mshambualiji Alexis Sanchez
wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kitakachoanza katika
mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa michuano ya Europa League dhidi
ya FC Cologne siku ya Alkhamis.
Wilshere hajawahi kucheza katika kikosi cha Arsenal tangu mwanzoni
mwa msimu huu, na ilidhamniwa huenda angeondoka kutoakana na changamoto
ya kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, alirejea klabuni hapo mwishoni
mwa msimu uliopita akiwa majeruhi, baada ya kumaliza mkataba wa mkopo wa
kuitumikia AFC Bournemouth.
Kwa mara ya mwisho aliitumikia Arsenal katika mchezo dhidi ya Watford miezi 13 iliyopita.
Kwa upande wa Sanchez ambaye alishindwa kufanikisha uhamisho wake wa
kuelekea Man city siku ya mwisho ya dirisha la usajili majira ya
kiangazi, alicheza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya AFC
Bournemouth akitokea benchi.
Katika hatua nyingine washambuliaji Theo Walcott, Olivier Giroud na
beki wa pembeni Mathieu Debuchy huenda wakapata nafasi ya kuanza katika
mchezo huo wa Europa League dhidi ya FC Cologne, ambao wanashika mkia
katika msimamo wa ligi ya nchini Ujerumani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Wilshere, Sanchez kuanza dhidi ya FC Cologne”
Post a Comment