Wednesday, September 13, 2017

Manchester United yarejea kwa kishindo UEFA


Manchester United imeanza vyema michuano ya UEFA Klabu Bingwa Ulaya kwa kuizaba FC Basel kwa mabao 3-0. Mchezo huo wa kwanza wa kundi A ulichezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
    Romelu Lukaku alipachika bao la pili
Bao la kwanza lilifungwa na Maroanne Fellaini ambaye alingia badala ya Paul Pogba aliyetoka kutokana na kujeruhiwa. Marcus Rashford ambaye alin'gara katika michuano ya Kombe la Europa, alianza michuano ya Ulaya kwa kufunga bao la tatu. Mchezo mwingine wa Kundi A ulikuwa kati ya Benfica na CSKA Moscow, ambapo wageni waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.
     Davide Zappacosta alipachika bao la pili
Mabingwa wa England Chelsea nao walianza michuano hii kwa kutoa kisago cha nguvu baada ya kuichapa FC Qarabag kwa magoli 6-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, London. magoli ya Chelsea yalifungwa na Pedro (dk 5), Zappacosta (dk 30), Azpilicueta (dk 55), Bakayoko (dk 71), Batshuayi (dk 76 na 82).
Kwingineko Paris Saint- Germain iliizaba Celtic mabao matano kwa sifuri, Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani wakicheka na nyavu katika mchezo wa kundi B. Bayern Munich pia walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Anderlecht.
Barcelona pia ilianza vizuri kwa kuichapa Juventus kwa magoli 3-0, Messi akifunga mawili na Ivan Rakitic la tatu. Sporting Lisbon wakicheza ugenini walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Olympiakos. Mcezo pekee uliomalizika bila magoli ulikuwa kati ya Roma dhidi ya Atletico Madrid.

0 Responses to “Manchester United yarejea kwa kishindo UEFA”

Post a Comment

More to Read