Sunday, September 10, 2017

SALASALA VISION GROUP NA UZALENDO WA KWELI


Picha ya Pamoja ya Salasala Vision Group nje ya Bunge Dodoma mara baada ya kusikiliza Bunge



Salasala Vision Group wakijipanga na Mchezo wao wakirafiki na wabunge


Salasala Vision Group wakiwa Bungeni kwa Mwaliko wa Spika wa Bunge mara Baada ya kutambua mchango wao katika Jamii

Moja ya barabara ambazo Salasala Vision Group wametengeneza.



Uzalendo limekuwa neno kuu katika siku za karibuni. Na wengi wetu tunatafsiri kama ni kuipenda na kuiweka Nchi yako mbele. Lakini sifa nyingine muhimu sana ya uzalendo ni kujitolea kwa faida au maendeleo ya wengi.

Salasala Vision Group ( SVG) iliasisiwa miaka 5 iliyopita na wakazi wachache wa Salasala Kilimahewa lengo likiwa ni kisaidia masuala ya ulinzi, mazingira, miundombinu, michezo na kuchochea maendeleo ya wanachama wake.

Hadi leo SVG imepanda miti zaidi ya 10,000, imetengeneza barabara za mitaa pamoja na kurekebisha barabara kuu, imetoa msaada vitendea kazi kwa polisi, kutengeneza viwanja vya michezo na pia kununua aridhi kwa wanachama wake zaidi ya hekari 250 huko Bagamoyo.

0 Responses to “SALASALA VISION GROUP NA UZALENDO WA KWELI”

Post a Comment

More to Read