Michezo
ROONEY,VAN PERSIE WAITETEA MAN U
.Mholanzi Robin van Persie alifunga bao la kwanza dakika ya 62 kwa penalti, kufuatia Chamakh kumchezea rafu Patrice Evra kwenye eneo la hatari.
Dakika sita baadaye, Muingereza Rooney akawainua vitini mashabiki wa United kwa bao safi la pili baada ya kupokea pasi ya Evra.
Ushindi huo, unaifanya United itimize pointi 45 baada ya kucheza mechi 27 na inarejea nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
IDADI KAMILI YA ASKARI WATAKAOLINDA USALAMA KOMBE LA DUNIA
Brazil imetangaza kwamba wameongeza maafisa wa kulinda usalama 70,000 zaidi watakao toa huduma za usalama katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
Idadi hii iliyoongezwa ni katika jitihada za kukabiliana na tishio la usalama na maandamano,idadi mpya iliyopendekezwa ni 100,000. .
Kwa ujumla maafisa wa usalama wapatao 170,000 watatumika katika miji 12 itakayoandaa mashindano hayo.
Jumatano wiki hii Rais wa Brazil Dilma Rouseff alisema kwamba jeshi litajumuishwa kwenye mpango huo dhabiti wa usalama iwapo kutaibuka wimbi lingine la maandamano.
Hatua hii inafuatia visa vya ghasia zilizoshuhudiwa katika miji tofauti tangu mwezi Juni mwaka uliyopita wakati Brazil ilipoandaa mchuano wa Kombe la Mashirika.
Mkuu wa Usalama wa Shrikisho la Soka Duniani FIFA amesema kuwa ana uhakika kwamba Brazil itaandaa michuano wenye usalama.
Kati ya idadi hiyo ya maafisa wa usalama, 150,000 watachaguliwa kutoka katika vikosi vya Polisi na mashirika mengine ya usalama huku wengine 20,000 watatoa huduma usalama ndani ya viwanja vyote 12.
Vikosi vya jeshi la wanamaji pia litazindua mazoezi ya kwanza kwa matayarisho ya dimba la Kombe la Dunia.
Operesheni hiyo maalum ya kupambana na ghasia inawahusisha wanajeshi 20,000, meli 60 na ndege 15 za kivita.
WAYNE ROONEY AONGEZA MKATABA WA KUBAKI MAN U HADI 2019
Wapenzi wa Manchester united hii itakuwa habari ya nzuri kwao kwasababu mtu muhimu kwenye kikosi chao amesaini mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.
Rooney amesaini mkataba wa kuendelea kuwa na club ya Manchester united kwa miaka 4 zaidi ambapo atakuwa hapo hadi 2019.
Picha kwenye instagram ya Man united ambayo inamuonyesha Rooney akisaini mkataba huo pembeni ya kocha wake imepewa caption hii “Great news for #mufc as Wayne Rooney signs a four-year contract extensionkeeping him at #mufc until June 2019.
UBAO WA KUANDIKIA MAGOLI WAZUA HOJA MBEYA
Hoja hiyo iliibukabaada ya wenyeji Tanzania Prisons kuwachapa wageni wao JKT Ruvu mabao sita kwa bila,na hatimae kukosekana tarakimu ya namba husika na kulazimika kutumia tarakimu mbili tofauti kwa wakati mmoja kama kuwakilisha namba husika kama ilivyo hapo juu.
Tukio hilo limeweza kukaa midomoni mwa washabiki wa soka wengi na kuwalazimu kutupia lawama hizo
zaidi kwa shirikisho la mpira wa miguu(TFF).
BARCA AMUUA CITY ETIHAD
Kuhadhirika huko kwa city kumesababishwa baada ya kupatikana kwa penalti iliyosababishwa na Messi kukatwa ndani ya boksi na Demichelis ambaye alipata kadi nyekundu baada ya kutenda dhambi hiyo,hapo ndipo Barca waliweza kuandika bao lao hilo la kwanza.
Baada ya mvutano wa dakika kadhaaa ndipo Dani Alvez aliweza kurudi tena kunako lango la City na kuweza kuiandikia Barca bao la pili'ambapo mabao hayo yaliweza kudumu mpaka mwishoni mwa mchezo na kuwatoa wakali hao wa Hispania kimasomaso.
Baada ya mvutano wa dakika kadhaaa ndipo Dani Alvez aliweza kurudi tena kunako lango la City na kuweza kuiandikia Barca bao la pili'ambapo mabao hayo yaliweza kudumu mpaka mwishoni mwa mchezo na kuwatoa wakali hao wa Hispania kimasomaso.
ARSENAL NA EVERTON ZATOSHANA NGUVU.
Mechi iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu na wapenzi wa mpira imemalizika kwa sale ya bao 1 - 1. wapenzi wengi wa mpira walikuwa wanasubiri matokea ya Arsenal na Everton kutokana na Munchester United kupokea kichapo cha goli moja bila na Everton wakiwa nyumbani kwao.
Katika dakika ya 80 mchezaji wa Arsenal OZIL aliiwezesha timu yake kuongoza kwa bao moja lakini katika dakika ya 84 Gerard Deulofeu alisawazisha goli hilo na kufanya mchezo kuwa sale hadi filimbi ya mwisho.
FULHAM YATOKA KIFUA MBELE
Fulham chini ya kocha wao mpya Rene Meulenstee imeifunga Aston Villa goli 2 - 0. Mabao hayo yalifungwa na Steve Sidwell katika dakika ya 21 ya kipindi cha kwanza na lengine lilifungwa na Dimitar Berbatov kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza.
MATOKEO YA MECHI ZA LEO LIGI KUU UINGEREZA.
Manchester United 0 - 1 Newcastle United.
Southampton 1 - 1 Manchester City
West Bromwich Albion 0 - 2 Norwich City
Stoke City 3 - 2 Chelsea
Liverpool 4 - 2 West Ham United
Crystal Palace 2 - 0 Cardiff City
MSIBA MWINGINE KWA MANCHESTER UNITED
Munchester United imepokea kichapo cha goli 1 – 0 katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Newcastle United ikiwani siku chache baada ya kufungwa na Everton goli 1 – 0. Yohane Cabaye ameifungia timu yake goli hilo katika dakika ya 61 ya kipindi cha pili. Goli hilo ni limevunja rekodi ya Newcastle United kutoifunga Manchester ikiwa kwao tangu mwaka 1972
Rio Ferdinand amamtupia lawama kocha wake David Moyes kwa uendeshaji wake wa timu hauko kama wa Sir Alex Ferguson kipinfi anawafundisha.
Kwa sasa Man U inashikiria nafasi ya 9 ikwa na pointi 22 tofauti ya pointi 12 na Arsenal ambao wanaongoza ligi hiyo Newcastle wako nafasi ya 6 wakiwa na na pointi 26.
KILIMANJARO STARS YAIONDOSHA UGANDA KATIKA KOMBE LA CECAFA
Timu ya Taifa ya Tanzania Kilimanjaro Stars imetinga nusu fainali baada ya kuifunga Uganda kwa mikwaju ya Penati. Mahamuzi ya kwenda kwenye matuta baada ya timu hzo mbili kuonyeshana nguvu katika dakika 90 za mchezo ambapo zilitoka sale ya mabao 2 – 2. Mrisho Ngassa alifungia mkilimanjaro stars magoli hayo uko Uganda ikifungiwa na Dan Sserenkuma pamoka na Martin Mpuga.
Dakika 30 ziliongezwa lakini hakuna tim iliyoweka bao langoni mwa goli la mwenzake. Emmanuel Okwi, Gor Mhia na Khalid waliipa tiketi Kilimanjaro star ya kwenda Nusu fainali huku stars ikikosa penati kwa mchezaji wao Kiiza Khamisi.
Matokeo hayo yameiwezesha stars kuingia katika Nusu fainali ya CECAFA akisubiri mshindi wa mechi zinzofatia kujua atacheza na nani? Katika kuwania nafasi ya kushiriki Nusu fainali.
TANZANIA USO KWA USO NA UGANDA
Timu ya Taifa ya Tanzania Kilimanjaro stars leo inashuka Dimbani kupapambana na Uganda kwenye robo fainali ya kombe la CECAFA mjini Mombasa Nairobi. Kilimanjaro stars inaingia dimbani kwa kupata nguvu nyingine ya kuongezeka kwa washambuliaji wao machachali Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Kilimanjaro stars imefuzu nafasi hyo baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Somalia bao moja bila ambapo timu ya Somalia ilionesha upinzani wa hali juu na kutoa matarajio ya watu wengi kuwa wao ni timu ya kubeza.
Timu nyingine zitakazo cheza robo fainali ya CECAFA ni KENYA vs RWANDA itakayochezwa leo baada ya mechi ya UGANDA vs KILIMANJARO STARS kufatiwa na mechi za kesho tarehe 8 Disemba 2013 kati ya ZAMBIA vs BURUNDI na baadae ETHIOPIA vs SUDAN.
TANZANITE KUIVAA AFRIKA KUSINI
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Tanzanite itashuka dimbani Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa saa kumi kukipiga na timu ya Afrka kusini maarufu kama Basetsana katika kufuzu mchujo wa kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri wa miaka ishirini (20)
Timu ya Afrika Kusini ya wasichana wenye umri wa chini ya miaka ishirini inaingia dimbani huku ikiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wao wa zamani Nelson Mandela. Itajua kama itaendeleza majonzi pamoja na kufungwa au kushinda kwa mechi ya kesho.
Kikosi cha Tanzanite kinachonolewa na Rogasian Kiajage amesema, tumejiandaa, vijana wako vizuri na wanasubiri saa ya mechi tu.
Mechi hiyo itahudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk, Fenella Mukangera. Viingilio vya mechi hiyo vitakuwa Tsh 1000 kwa viti vya kijani, Blue na Orange, Tsh 2000 ni VIP C,Tsh 5000 VIP B, Tsh10000 ni VIP A tiketi zinapatikana mlangoni.
MAKOCHA WAZUNGUMZA JUU YA MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA
Makocha thelathini na mbili wa Timu za kombe la dunia wakiwa katika picha ya pamoja.
GROUP A
|
GROUP B
|
GROUP C
|
GROUP D
|
Brazil
|
Spain
|
Colombia
|
Uruguay
|
Croatia
|
Nethlands
|
Greece
|
Costa Rica
|
Mexico
|
Chile
|
Cote D Ivoer
|
England
|
Cameroon
|
Australia
|
Japan
|
Italy
|
GROUP E
|
GROUP F
|
GROUP G
|
GROUP H
|
Switzerland
|
Argentina
|
Germany
|
Belgium
|
Ecudor
|
Bosnia -Herzegovina
|
Portugal
|
Algeria
|
France
|
Iran
|
Ghana
|
Russia
|
Honduras
|
Nigeria
|
USA
|
Korea
|
Kocha Fabio Capello wa England amesema kundi
waliokuwepo ni jepesi kulinganisha na Makundi kama kundi B na Kundi G na
kutumai kuongoza kundi hilo. Wakati Capello anasema hayo Mshambuliaje wake
Wayne Rooney ameibuka akisema kama wanataka kuwa wa kwanza wanatakiwa kuzifunga
timu bora aidha aliongeza kwa kusema ni kundi lao ni gumu.
Scolari amesema amelidhika na droo iliofanyika na
watatilia mkazo mechi zao za mwanzo
Kwasi Appiah Kocha wa Ghana amesema ni vizury
tumekutana tena na timu za mwaka 2010 katika kombe la Dunia liliofanyika Afrika
kusini ambazo ni Germany na USA, naamini tuko vizuri zaidi ya mwaka 2010,
Aidha ndugu wawili mtu na kaka yake Jerome Boteng na Kevin Boteng wanakutana tena kwa mara ya pili kwenye kombe la dunia la mwaka 2014 kama walivyokutana katika kombea la Dunia lililofanyika Afrika kusini.
9:27 PM by Unknown · 0
Subscribe to:
Comments (Atom)


.gif)








.jpeg)

0 Responses to “Michezo”
Post a Comment