Tuesday, March 11, 2014

MCHUNGAJI MTIKILA AMRIPOKEA PANDU KIFICHO, ADAI ANAMNYIMA KUZUNGUMZA BUNGENI.





Mchungaji Christopher Mtikila amechafua hali ya hewa bungeni, kwa kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Kificho amueleza ni kwanini tangu jana amekuwa  akimnyima nafasi ya kuzungumza bungeni. 
 
Mchungaji Mtikila alisimama ghafla na kusema: Mwenyekiti kwanini unaninyima haki yangu ya kuzungumza, nataka kujua kwanini unaninyima haki ya kuzungumza. Kuzungumza ni haki yangu."

Mchungaji Mtikila amezungumza kwa jazba huku wajumbe wengine wakimzomea, lakini bila uwoga aliendelea kuzungumza na kusema yanayofanyika Mungu anapenda na yeye ana amini katika Mungu, lakini "Wewe Mwenyekiti inaonekana kuwa hupendi Mungu."

Wakati Mchungaji Mtikila akimwakia Kificho, Felix Mkosamali alilipuka na kumwambia mwenyekiti kuwa tangu jana pia anamnyima nafasi.

"Ninyi mmejipanga, kupitisha kanuni mbovu, alafu sisi wengine hamtupi nafasi," amesema Mkosamali.

Mwenyekiti Kificho aliwajibu kuwa kwa bahati mbaya wamekosa nafasi Kutokana walioomba kuchangia kuwa wengi na hivyo wawe wavumilivu.

0 Responses to “MCHUNGAJI MTIKILA AMRIPOKEA PANDU KIFICHO, ADAI ANAMNYIMA KUZUNGUMZA BUNGENI.”

Post a Comment

More to Read