Tuesday, March 11, 2014
WAZAZI WA MTOTO ANAYEHITAJI MSAADA WAKO ILI APATIWE MATIBABU WAWASILI MKOANI MBEYA.
Do you like this story?
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi. TUNAOMBA SANA MSAADA WENU MTOTO ATIBIWE KWANI ANATESEKA SANA MTOTO HUYU
|
Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbani. |
Mama mzazi wa Adorotea Milika Kibelege. |
Hatimaye Wazazi wa mtoto Adorotea
Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne wamewasili Jijini Mbeya
kutoka Mkoani Njombe baada ya kutafutwa kwa muda mrefu kutolea maelezo ya ajali
ya mtoto aliyeungua moto miezi saba iliyopita.
Ajali hiyo imepelekea ulemavu mkubwa
kwa mtoto huyo ambapo ngozi ya kidevu imeungana na kifua na kumsababishia ulemavu
unaomfanya kushindwa kula vizuri na macho kushindwa kufumba.
Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike
amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbani kwani mtoto alibaki na
mama yake mzazi aitwaye Milika Kibelege.
Milika amesema kwamba ajali hiyo
ilitokea majira ya saa mbili usiku alipokuwa anapika na yeye kupigwa na kitu
kichwani kisha mtoto kudondokea motoni nay eye kuzirai kabla ya mtoto kuokolewa
na majirani baada ya kusikia kilio kikali kutoka kwa mtoto.
Milika amesema kuwa baada ya
tukio mtoto alikuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji cha Wanzali na
kwamba yeye alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo hali iliyomlazimu Dada yake
kumchukua mwanae hadi Mbeya ili aweze kupatiwa matibabu zaidi.
Kutokana na uduni wa maisha wameshindwa
kufika Mbeya kumjulia hali mtoto wao hadi walipofuatwa na Dada yake Machi 8
mwaka huu kuwa wanahitajika Mbeya ili kibali kitolewe mtoto asafirishwe
kwenda Hospitali ya Mhimbili kwa matibabu zaidi.
Mama Mkubwa
wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye alitoweka na
mtoto huyo amesema anaomba radhi kwa kuondoka bila kuaga na mtoto huyo kwani
alichanganyikiwa alipoambiwa mtoto itabidi asafirishwe kwenda India na matibabu
yake yatachukua miezi sita hivyo akaona ni bora awafuate wazazi wa mtoto huko
njombe wakajadiliane
Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya
Thobias Mwalyego baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari
alilazimika kwenda hadi mtaa wa Maendeleo Iyunga ili kupata maelezo ya kina
kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtoto huyo.
Mwalyego amesema kuwa kuanzia sasa
ataendelea kufuatilia maendeleo ya mtoto huyo kuhakikisha anapatiwa huduma
zinzostahili ukiwemo msamaha wa matibabu kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa upande wa wazazi wamewashukuru
wasamaria wema waliojitokeza kuchangia matibabu ya mtoto wao na madaktari
wanaofanya juhudi za kuhakikisha mtoto huyo anapatiwa upasuaji wa haraka.
Aidha amekubali kuandamana na mwanae
katika matibabu endapo ataruhusiwa kwenda kokote na Afisa Ustawi wa Jamii
alishauri pia Mama mkubwa kuongozana na Familia hiyo kutokana na udhaifu wa
mama Adorotea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZAZI WA MTOTO ANAYEHITAJI MSAADA WAKO ILI APATIWE MATIBABU WAWASILI MKOANI MBEYA.”
Post a Comment