Friday, March 21, 2014

MKUU WA MKOA WA NJOMBE ARUDIA AGIZO LA SERIKALI LA KUPIGA MARUFUKU KUWAFUKUZA WANAFUNZI KUFUATA MICHANGO.


 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Ilembula Leo wakati Akihitimisha Ziara yake ya siku tatu Wilayani Wanging'ombe  Mkoani  Njombe.



Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain  Mstaafu Asseri Msangi Amerejea Kauli  Ya Serikali ya Kupiga Marufuku Kitendo cha Walimu Kuwarudisha Wanafunzi Kufuatia Michango Ya Aina Yoyote Ile Kufuatia Kuwepo Kwa Baadhi ya Malalamiko Ya Wazazi Katika Shule za Msingi na Sekondari Katika Kata ya Ilembula.

Kauli Hiyo ameitoa Leo Wakati Akihitimisha Ziara ya Siku Tatu Wilayani Wanging'ombe Akiwa Katika Kijiji cha Igelehedza Kata ya Ilembula Wilayani Humo Baada Ya Baadhi ya Wazazi Kulalamikiwa Kitendo cha Walimu Kuwafukuza Wanafunzi Kwenda Kufuata Michango Hali Iliyotajwa Kuongeza Usumbufu Kwa Wazazi na Kushusha Kiwango Cha
Elimu Hapa Nchini. Baadhi ya Wazazi Hao Wamesema Kuwa Licha Ya Serikali Kupiga Marufuku Kitendo Hicho Lakini Baadhi ya Shule Zimekuwa Zikiendelea Kukiuka Agizo Hilo na Kisha Kuendelea Kuwafukuza Watoto.

Kufuatia Malalamiko Hayo,Mkuu wa Mkoa wa Njombe Akamtaka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Igelehedza Bwana Wistoni Chalangwe Kujibia Malalamiko Hayo Ambaye Amekanusha Tuhuma Hizo za Kuwafukuza Wanafunzi Hao Huku Akisema Kuwa Kumekuwepo Kwa Michango Ya Aina Tofauti Ikiwemo Inayoanzishwa Kwa Mujibu wa Kamati za Shule na Wazazi .

Kutokana na Majibu Hayo Ndipo Mkuu wa Mkoa Wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Ndipo Akirejea Kauli Hiyo Ya Serikali Ya Kupiga Marufuku Kitendo Cha Walimu Kuwafukuza Wanafunzi Kwenda Kufuata Michango Hiyo.

Pamoja na Mambo Mengine Mkuu Huyo wa Mkoa Akiongozana na Baadhi ya Wataalamu wa Sekretarieti Ya Mkoa na Watumishi wa Halmashauri Ya Wilaya ya Wanging'ombe Pamoja na Mkuu wa Wilaya,Mwenyekiti wa Halmashauri na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe Ameagiza Kuhakikisha Agizo la Rais Kikwete la Kujengwa Kwa Maabara Tatu Kila Shule ya Sekondari Ifikapo Mwezi Disemba Mwaka Huu Linakamilika Kwa Namna Yoyote Ile.

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA NJOMBE ARUDIA AGIZO LA SERIKALI LA KUPIGA MARUFUKU KUWAFUKUZA WANAFUNZI KUFUATA MICHANGO.”

Post a Comment

More to Read