Thursday, March 20, 2014
KENYA YATOA UZOEFU KWA BUNGE NLA TANZANIA.
Do you like this story?
Bunge la Tanzania likiwa kwenye vikao vyake |
Ujumbe maalum kutoka nchini Kenya
umehutubia wajumbe wa Bunge la Katiba nchini Tanzania kuelezea uzoefu wao
kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya nchini Kenya ulivyofanyika.
Akizungumza na Wajumbe wa Bunge
maalum la katiba, Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Kenya,Amos Wako ameainisha
masuala ya msingi ya kuzingatia katika upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania.
Bwana Wako ameeleza uzoefu wake wa
upatikanaji wa katiba ikizingatiwa kuwa wakati mchakato wa kupata katiba mpya
nchini Kenya alikuwa miongoni mwa watendaji wakuuu wa mchakato huo akiwa
mwanasheria mkuu wa serikali.
Bwana Wako amewataka wajumbe wa
bunge maalum la katiba nchini Tanzania kuzingatia historia, utamaduni na
matakwa ya watanzania.
Wako amesema kuwa baada ya machafuko
ya nchini Kenya na jumuia ya kimataifa kuingilia kati, mapendekezo yaliyotolewa
na kamati ya usuluhishi iliyoongozwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa
Mataifa Koffi Annan yaliona kuwa suala la kupata Katiba mpya nchini Kenya,
lichukuliwe kuwa suala la Haraka na dharura.
Semina hii kwa Wajumbe wa Bunge la
katiba imekuja wakati Rais wa Tanzania Jakaya kikwete akitarajiwa kufungua
rasmi Bunge maalum la Katiba siku ya Ijumaa mjini Dodoma katikati mwa Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KENYA YATOA UZOEFU KWA BUNGE NLA TANZANIA.”
Post a Comment