Thursday, March 20, 2014

POLISI MBEZI WADAIWA KUUMA FUNDI UJENZI.


 Kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni camilius wambura
 


Polisi wa kituo cha Mbezi  kwa yusuph jijini dar es salaam, wanadaiiwa  kumuua  kwa kumpiga fundi ujenzi aliyetajwa  kwa jna la elinema massawe.

Binamu wa marehemu, Gilbeth  mushi amesema jana kuwa kifo cha ndugu yake  kimetokana na kipigo  alichopata kutoka kwa askari wa kituo hicho ingawa polisi mkoa wa kinondoni  imesema inachunguza  suala  hilo.

Walimkamata ijumaa iliopita  akiwa mzima kwenye shughuli  zake za ujenzi mbezi. Walimhuisha na tukio la wizi wa gari, wakampeleka kituoni alipopigwa  vikali sehemu  mbalimbali mwilini amesema binamu.

Walimvunja miguu kutokana na kipigo, mke wake aliwaomba wamruhusu akatibiwe lakini askari walimkamata  mpaka  juzi walipoona hali yake mbaya ndipo wakamruhusu akiwa chini ya ulinzi.

Mushi amesema ndugu yake alifariki dunia kabla ya kuanza kupewa matibabu katika  hospitali ya tumbi, kibaha  na sababu kubwa ni kupoteza  damu nyingi kutokana na majeraha  aliyoyapata.

Imeniuma sana askari  tuliyekwenda naye hospitali alidanganya kwa muuguzi kwa kusema marehemu alikuwa kwenye hali mbaya kutokana na kipigo  kutoka kwa wananchi, alisme mushi.

Kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni camilius wambura amesema taarifa  kuhusiana na kifo cha elinema amezipata .

Suala la kufa mtu lazima liangaliwe kwa makini ili kujua sababu za kweli za kifo. Tunataka kujua wapi alipokamatwa  na katika  mazingira  gani.

Tunaendelea kuchunguza kwa kina kasha tunatoa taarifa alisema wambura.

0 Responses to “POLISI MBEZI WADAIWA KUUMA FUNDI UJENZI.”

Post a Comment

More to Read