Thursday, March 20, 2014

MTUHUMIWA DAWA ZA KULEVYA ATOA KETE 82.





Kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya nchini kimesema  mtuhumiwa  mashusha  matata hadi sasa ameshatoa kete 82  za dawa  ya kulevya aina cocaine zenye thamani y ash 83.6 millioni.

Matata alikamatwa machi 17  mwaka huu, saa 8 mchana  katika uwanja wa ndege  wa kimataifa wa Julius nyerere  akitoka brazil  alitua na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia.

Akizungumza jana kamanda wa kitengo hicho godfredy nzowa alisema awali mtuhumiwa alitoa kete 21  kwa njia ya haja kubwa.

Kamanda nzowa amesema  matata alitoa kete hizo kwa awamu  tatu kwanza kete 30  baadaye kete 31  siku inayofuata alitoa kete 21.

Amesema mtuhumiwa huyo akiwa na hati ya kusafiria yenye namba AB362172  mali ya Tanzania alitiliwa shaka na askari polisi hivyo kumtia nguvuni.

Aliposhuka uwanja wa ndege tulimshuku huenda akawa amebeba dawa za kulevya. Tuliamua kumhoji kabla ya kuja kukubali saa moja baadaye amesema nzowa.

Kamanda nzowa amesema bado wanaendelea na upelelezi na kwamba hatua hiyo itakapo kamilka atasomewa mashataka mahakama kuu kwa vile thamani ya dawa hizo  ni kubwa na mtuhumiwa bado anaendelea kuzitoa.
  

0 Responses to “MTUHUMIWA DAWA ZA KULEVYA ATOA KETE 82.”

Post a Comment

More to Read