Thursday, March 20, 2014

SULUHU: NITAFUATA NYAYO ZA ATTAH MILLS.


Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba samia suluhu Hassan.



Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba samia suluhu Hassan amesema atatumia mtindo  wa aliyekuwa Rais wa Ghana  hayati Profesa John Attah Mills kwenye mijadala ya kuboresha rasimu za katiba bungeni ili kujiandalia mazingira mazuri ya maisha yake ya baadaye.

Kauli hiyo inalenga kuunga mkoni jitihada za wawakilishi wa jumuiya wa wazee Tanzania  waliofika ofisini kwake bungeni kuwasilisha maombi  yao ya kutaka wabunge kuzingatia haki zao wakati wakitelekeza majukumu hayo .

Msafara wa wazee hao ulliongozwa na  mwenyekiti wa jumuiya hiyo Sebastian  bulega na katibu  wa jumuiya ya wastaafu na wazee Zanzibar , DK yusuf Nuh Pandu  uliomba katiba ijayo itoe tafsiri ya mzee kuwa ni mwanamke au mwanaume mwenye umri wa mika a kuanzia 60.

Bulega lisema wanataka ibara ya 10(iv)  iliyo kwenye rasimu ibakizwe  na ili itekelezwe  vizuri walitaka tafsiri ya mzee kwa maana ya umri iainishwe . ibara hiyo ipo kwenye sura  ya pili inayohusu malengo, misingi ya mwelekeo  wa shughuli za serikali na sra za kimataifa.

0 Responses to “SULUHU: NITAFUATA NYAYO ZA ATTAH MILLS.”

Post a Comment

More to Read