Thursday, March 20, 2014
AJERUHIWA BAADA YA KUMWAGIWA MAFUTA YA KULA MWILINI KUTOKANA NA MGOGORO WA NDOA MBEYA.
Do you like this story?
Lugano Mwambuja(50) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Sange iliyopo Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya. akiwa amelala nyumbani kwake akiuguzwa majeraha ya moto |
Mama mzazi Lugano akimuuguza mwanaye. |
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mwanamke mmoja
Mkazi wa Mtaa wa Ilembo kata ya Iyela Jijini Mbeya amemjeruhi mume
wake baada ya kumwagia mafuta ya moto kichwani kwa kile kilichodaiwa kuwa
ni mgogoro wa ndoa baina yao.
Mwanamke huyo
aliyefahamika kwa jina la Beatrice Lusamba (37) alitenda tukio hilo mwishoni
mwa wiki majira ya saa saba mchana ambapo alimwagia mafuta hayo Mume wake
Lugano Mwambuja(50) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Sange iliyopo
Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.
Akizungumzia
tukio hilo Mhanga wa kisa hicho alisema yeye makazi yake yako Wilayani Ileje
lakini Mkewe pamoja na baadhi ya watoto wake huishi Jijini Mbeya hivyo hufika
nyumbani hapo mara chache kwa ajili ya kutembelea familia na kupeleka huduma
mbali mbali kama baba wa familia.
alisema siku
ya tukio alialikwa na Mkewe huyo kula chakula cha mchana ambapo baada ya
kukaribishwa ndani mwanamke huyo aliingia jikoni akiwa na mayai matatu na
galoni la mafuta ya kupikia, ambapo yeye alibaki Sebureni akisubiri chakula
alichokaribishwa apikiwe.
Alisema baada
ya dakika kumi Mkewe huyo alirejea Sebuleni akiwa ameshika kikombe chenye
mafuta yaliyochemshwa ambayo alimwagia mwilini na kisha kukimbilia nje
akimwacha mumewe akiugulia maumivu makali yaliyotokana na kuungua na mafuta ya
moto mwilini mwake.
Mwalimu huyo
aliongeza kuwa baada ya kupiga kelele ya kuomba msaada ndipo alipojitokeza
jirani yake aliyefahamika kwa jina la Andamisye Kajange ambaye baada ya kumuona
katika hali hiyo alimkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya alikopatiwa
matibabu na kuruhusiwa.
Mjumbe wa
Mtaa Ilembo, Philly Mwakapimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza
kuwa kabla ya kupeleka Hospitali Mhanga waliripoti Kituo cha Polisi na kupewa
fomu namba tatu (PF3) pamoja na kufungua faili namba IR/2253/2014 na
kuendelea kutibiwa.
Aliongeza
kuwa mtuhumiwa hajakamatwa hadi leo baada ya kutorokea kusikojulikana huku
lawama likipewa Jeshi la Polisi kutokana na kushindwa kumkamata mtuhumiwa kwa
wakati hadi anapata mwanya wa kutoweka katika eneo la tukio.
Akizungumzia
mahusiano yake na mkewe Mwalimu huyo alisema alioana na mkewe mwaka 2007 kwa
ndoa ya kimila baada ya kufiwa na mkewe wa awali mwaka 2006 alimyemwachia
watoto wawili ambao ni Doris(20) na Happy Mwambuja(21) ambapo aliamua kuoa mke
huyo kwa ajili ya kusaidia malezi ya watoto hao.
Alisema akiwa
kazini mara nyingi alikuwa akipata taarifa za mgogoro kati ya mkewe huyo na
watoto jambo lililosababisha usuluhishi wa mara kwa mara kufanyika ukiongozwa
na Serikali ya Mtaa huku sababu ikibainika kuwa ni tamaa ya mwanamke huyo
kutaka kumiliki Nyumba ya Mwalimu huyo ili iwe mikononi mwake na siyo Familia.
Alisema mara
nyingi Mwanamke huyo amekuwa akijaribu kuiba hati ya nyumba ili abadilishe
majina na umiliki lakini anashindwa hali iliyoml;azimu Mwalimu huyo kuamua
kununua eneo lingine na kujenga ili kumtengnisha mkewe pamoja na watoto lakini
hali bado ilikuwa tete baada ya mwanamke huyo kutaka amilikishwe yeye nyumba.
hadi sasa
Mwalimu huyo anaendelea kupatiwa matibabu Nyumbani kwake huku Jeshi la Polisi
likiendelea kumsaka mtuhumiwa kwa ajili ya kumfikisha katika vyombo vya sheria
kujibu shtaka la kujeruhi kwa makusudi.
mwisho.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AJERUHIWA BAADA YA KUMWAGIWA MAFUTA YA KULA MWILINI KUTOKANA NA MGOGORO WA NDOA MBEYA.”
Post a Comment