Friday, March 7, 2014
WANANCHI WAKATISHWA TAMAA NA BUNGE LA KATIBA.
Do you like this story?
Wananchi
kadhaa wameeleza kusikitishwa na mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba, huku
wakimtaka Rais Jakaya Kikwete aikemee hali hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen-Kijo
Bisimba, amesema, ni aibu kwa kinachoendelea katika bunge hilo.
“Leo
(jana) niliacha kazi zangu na kujipa muda wa kuangalia shughuli ya hilo bunge
na kwa kweli nimeishia kuwa dis-appointed (nimekatishwa tama) na nilichokiona,
kiasi cha kuandika kwenye ukurasa wetu wa face book,” amesema.
Amesema
alishangaa sana jinsi wajumbe wanavyozomeana, kiasi cha kutomsikiliza hata
mwenyekiti, kinyume na utaratibu unaowataka wajumbe wakae pale mwenyekiti
anaposimama.
“Mivutano
yao haina tija na badala yake wanapoteza hela za Watanzania bure…yaani kama kwa
kipindi chote cha wiki tatu bado wanahangaika na kanuni, itakuwaje wakiifikia
rasimu yenyewe,” alisema.
Dk.
Bisimba amesema ili kuwaweka kwenye msitari, ni wakati wa Rais Kikwete
aliyewateua sasa kuikemea hali, ili warudi kufanya kazi iliyowapeleka ya
kutupatia katiba tunayoitaka.
Profesa
Mwesiga Baregu alisema hali hiyo inatokana na wajumbe kutopata semina ya
kuwaandaa.
“Tungekwenda
sawa kama wangepata semina ya kuwafunda ili wajue kilichowapeleka kule, na kitu
gani wananchi wanakitarajia kutoka kwao, bahati mbaya haikuwepo,” alisema na
kwua kinachoonekana katika kadhia hiyo, ni kutokuwepo kwa ratiba ya kuliongoza
hilo bunge.
“Nasema
hivyo kwa sababu ukiwa na ratiba, itakuongoza katika shughuli zako kwa kuwa
utaangalia shughuli ulizo nazo na muda ulio nao, na itakusaidia kujitathmini
kama unaenda vizuri,” alisema.
Mhadhiri
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema mambo
yanayofanyika Dodoma katika Bunge la Katiba yanawahuzunisha wananchi.
Pia,
amesema bunge hilo halikufanyiwa maandalizi mazuri kabla ya kuanza na ndiyo
maana mambo hayo yanatokea.
Aidha,
Dk. Bana amesema Bunge hilo linayumba kwa sababu bado halijapata Mwenyekiti wa
kudumu na kwamba anaamini akipatikana Mwenyekiti wa kudumu litatulia na
kuendeshwa vizuri.
Aliitaka
Kamati inayomshauri Mwenyekiti wa muda izingatie suala la muda kwa sababu
kuahirishaahirisha kunaweza kuchelewesha kufanikisha shughuli hiyo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, alisema wabunge
wanatakiwa kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili waweze kufanikisha kazi
hiyo.
Amesema
watanzania wanahitaji kupata Katiba nzuri, lakini wabunge wa bunge hilo
wanatakiwa kuzingatia muda na kutolifanya bunge hilo kuwa mzigo mkubwa kwa kuwa
gharama inayotumika ni kubwa.
“Naelewa
umuhimu wa kupata muafaka, lakini ninaomba usicheleweshwe sana na ukasababisha
mambo mengine yashindwe kufanyika, wakumbuke pia kwamba hapo baadae watahitaji
kuingia katika bunge la bajeti,” amesema Kinana na kuongeza.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, alisema tatizo kubwa
linalosabisha kutokea kwa vurugu katika bunge hilo ni kutokana na wajumbe
kutakunguliza maslahi ya vyama vyao na kusahau kwamba kilichowapeleka ni kwa
ajili ya Watanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANANCHI WAKATISHWA TAMAA NA BUNGE LA KATIBA.”
Post a Comment