Mtuhumiwa wa
wizi baada ya kupewa kichapo na wananchi, hapa ni kabla hajauawa. Kipigo
kikiendelea. Wananchi wakiwa wamemzunguka mtuhumiwa huyo wa wizi huku
akiendelea kupigwa.
Wananchi wenye hasira katika kata ya Tandala
wilayani Makete mkoa wa Njombe wameamua kujichukulia sheria mkononi, kwa
kumpiga hadi kumuua kinyama mtuhumiwa wa wizi ambaye walimkamata kwa madai kuwa
ni mwizi wa mifugo Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao walikataa kutaja majina yao wala
kupigwa picha, wamesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji cha Idege,
ambapo kwa madai yao walimkamata na vithibitisho ambavyo ni kamba.
|
0 Responses to “WANANCHI WAMPIGA HADI KUMUUA KINYAMA MTUHUMIWA WA WIZI WILAYANI MAKETE”
Post a Comment