Sunday, April 27, 2014
CHELSEA YAIADHIBU LIVERPOOL 2-O
Do you like this story?
Chelsea
vijana wa darajani Stanford, jijini London, wamewanyamazisha vinara wa ligi kuu
ya England, Liverpool baada ya kuwachakaza mabao 2-0 katika uwanja wao wa
Anfield.
Liverpool
ikiwa imeuanza mchezo huo kwa kasi na kwa dhamira ya kupata ushindi ilishuhudia
jahazi lake likitota katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.
Alikuwa
ni Demba Ba aliyeanza kupeleka kilio kwa majogoo wa Liverpool pale alipounasa
mpira kufuatia nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kuteleza na Ba kupata mwanya
wa kumfunga kirahisi Mignolet.
Liverpool
hawakukubali kusalimu amri kwa wageni,kwani waliendelea kupeleka mashumbulizi
ya hatari langoni mwa wapinzani wao wakiishia kwa kosa kosa. Liverpool
wanapigania ubingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza katika miaka 24
iliyopita.
Joe
Allen na Luis Suarez walizidisha mashambulizi katika lango la Chelsea, kabla ya
Willian aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la pili kwa timu yake ya
Chelsea baada ya Fernando Torres bila uchoyo akiwa katika nafasi ya kufunga
alimpasia Willian na kuwaachia kilio wenyeji wao Liverpool.
Chelsea
katika mchezo huo ilikuwa ikipewa nafasi finyu ya kuibuka washindi. Lakini ni
Jose Mourinho aliyeibuka na kicheko, huku Brendan Rodgers akiugulia kipigo cha
kwanza kwa timu yake tangu kuanza kwa mwaka huu.
Kwa
ushindi huo sasa, Chelsea inaachwa pointi mbili nyuma ya Liverpool ambayo
inaoongoza ikiwa na pointi 80, baada ya michezo 36. Msimamo wa timu hizo ni
Liverpool pointi 80, Chelsea 78, Manchester City 74, itakuwa na pointi 77 iwapo
itaifunga Crystal Palace katika mchezo wao, huku Arsenal ikichukua nafasi ya
nne ikiwa na pointi 70. Manchester City na Arsenal zimecheza mechi 35 kila moja
huku Liverpool na Chelsea zikiwa zimecheza mchezo mmoja zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CHELSEA YAIADHIBU LIVERPOOL 2-O”
Post a Comment