Monday, April 7, 2014
MATUMAINI KATIBA MPYA ARIJOJO.
Do you like this story?
Ikulu imeeleza kuwa imeshindwa kutimiza ahadi
yake kwa taifa ya kulipatia Katiba Mpya ifikapo Aprili 26, 2014.
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni
Sefue Alieleza kuwa kwa hali ya mchakato huo ilivyo sasa, wameshindwa kufikia
lengo hilo, lakini hawajakata tamaa kuhusu kupatikana Katiba Mpya ndani ya
mwaka huu.
“Kweli matarajio ya awali yalikuwa hayo,
lakini kama unavyoona hali ilivyo, ni vigumu kusema matarajio mengine, ingawa
majadiliano yaliyofanywa mwaka huu ni lazima Katiba inayopendekezwa iwasilishwe
kwa wananchi na mwakani tutakuwa na Katiba Mpya,” alieleza Balozi Sefue.
Katika hali isiyoeleweka Balozi Sefue
alisisitiza msimamo wa awali wa Serikali kwamba Katiba itakayopatikana
itatumika kwenye Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na
Demokrasia (Chadema), Dk. Willbroad Slaa, alisema hilo ni fundisho kwa Serikali
kwamba kiburi na jeuri havitakiwi katika masuala yanayohusu umma.
Alisema muda huo wa kupatikana Katiba Mpya
ulipotangazwa, walioanzisha kilio cha kudai Katiba Mpya nchini ambao aliwataja
kuwa ni vyama vya upinzani vya siasa, taasisi mbalimbali za kijamii walipinga
na kutoa ushauri kwa Serikali, lakini walipuuzwa.
Dk. Slaa alisema walipendekeza kwamba badala
ya kupeleka mchakato wa Katiba mchakamchaka, warekebishe kwa mara ya 15 Katiba
inayotumika, ili iende na wakati wa sasa ikiwamo Uchaguzi Mkuu ujao kwa lengo
la kutoa muda wa kutosha kwa mchakato wa taifa kupata Katiba Mpya.
“Lakini walitukebehi na kututukana sana, sasa
kiko wapi Aprili 26 hiyo hapo na Katiba haijapatikana na kusema itapatikana
mwaka huu na kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani ni ndoto za mchana,”
alieleza Dk. Slaa.
Dk. Slaa alisema tukio hilo liwe fundisho kwa
Serikali, wawe wakweli, wanyoofu na wafahamu kuwa nje ya Serikali kuna watu
makini na wanaojua vilivyo mchakato wa Katiba.
Alisema ana taarifa za Bunge Maalumu
kuahirishwa Mei 9, 2014 ili kupisha Bunge la Bajeti. Hivyo mategemeo ya Katiba
Mpya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, yanatia shaka.
“Kwa akili ya kawaida tu isiyohitaji elimu ya
chuo chochote, kutumia Katiba Mpya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao ni jambo
lisilowezekana kwa hiyo waache kutuletea matumaini yasiyokuwapo, sisi siyo
watoto wadogo,” alieleza Dk. Slaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MATUMAINI KATIBA MPYA ARIJOJO.”
Post a Comment