Monday, April 7, 2014
SIMBA,MBEYA CITY VITANI.
Do you like this story?
Mbeya City wataishusha Yanga
katika nafasi ya pili kama wataibuka na ushindi leo dhidi ya Ashanti United
kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, huku Simba wakiwa na kibarua
kizito mbele ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Mbeya City ipo katika nafasi ya tatu kwenye
msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 45, wakati Yanga inakamata nafasi ya pili
ikiwa na pointi 46 na Azam FC inayoshikilia uongozi wa ligi ikiwa na
pointi pointi 53.
Endapo Mbeya City itaifunga Ashanti leo
itafikisha pointi 49, hivyo kuchumpa katika nafasi ya pili na kuishusha Yanga
itakayoumana na JKT Ruvu kesho katika nafasi ya tatu.
Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema
hana muda wa kupoteza zaidi ya kuhakikisha anatoa adhabu kali kwa kila timu
atakayokutana nayo kuanzia na Ashanti.
“Tumejizatiti kikamilifu kuhakikisha tunaibuka
na ushindi katika mechi zetu zote zilizosalia ili atakayeteleza tu basi
tunyakue nafasi moja kati ya mbili za juu,” alisema Mwambusi.
Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibadeni anaingia
kwenye mchezo huo akijua wazi kipigo kitazidi kuwaweka katika hatari zaidi ya
kushuka daraja msimu huu.
Kibadeni amekiri kwamba mambo yamezidi kuwa
magumu na kwamba kubaki kwa timu yake katika ligi kuu kutategemea kudra za
Mwenyezi Mungu.
“Kuna timu sita za majeshi ambazo hizi zote
ni jamii moja hapo unategemea sisi (Ashanti) tutapona kweli? angalia kwenye
msimamo juu yetu zipo JKT Mgambo, Prisons na JKT Ruvu ambazo ni rahisi kabisa
kwao kubebana, sasa tutahakikisha mechi tatu zilizosalia tunashinda halafu
tuone tunakuwa katika nafasi ipi,”alisema Kibadeni.
Patashika nyingine leo ni ile ya Simba
itakayojitupa uwanjani kukwaana na Kagera Sugar katika pambano litakalopigwa
kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Simba wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo
ili kulinda heshima yao baada ya kutimuliwa katika mbio za kusaka nafasi mbili
muhimu za juu, yaani ubingwa au mshindi wa pili.
Kikosi hicho cha kocha Zravko Logarusic
kinakamata nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kikiwa kimejikusanyia pointi 36
kupitia mechi 23, Kagera Sugar ipo katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 33.
Simba imeondoka na wachezaji 19, huku
ikiwaacha Amis Tambwe, Joseph Owino, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Abdulhalim Humud
na Betram Mwombeki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA,MBEYA CITY VITANI.”
Post a Comment