Monday, April 7, 2014
MSEKWA:SITTA ANA LAKE JAMBO.
Do you like this story?
Siku moja baada ya Mwenyekiti
wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta kukiri kuchezewa kwa saini ya aliyekuwa
Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere, Msekwa amesema, ‘mzungumzaji huyo ana lake jambo’.
Sitta akizungumza na gazeti hili juzi mjini
Dodoma alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya
1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.
Alifafanua kuwa saini ya Nyerere imeongezwa
herufi ‘us’ kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno
‘Msekwa’ kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno
hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona
sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.
Msekwa akizungumza na gazeti hili jana
alisema: “Saini iliyo katika hati original (halisi) ni ya kwangu mimi, lakini
huyo anayesema zimechezewa muulizeni atakuwa na lake jambo. Kama kompyuta
imekosea ni leo kwa kuwa kipindi hicho kompyuta hazikuwapo.”
Aliongeza: “Ana lengo gani la kutilia shaka,
ana lengo gani la kusema imechakachuliwa, kinachotakiwa ni hati original ambayo
iko ofisi ya Katibu wa Bunge itolewe, kwanini tuendelee kuandikia mate wakati
wino upo?”
Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Taarifa kwa
Wananchi Umma (TCIB), Hebron Mwakagenda alisema yote hayo yanatokea ni kuvuruga
hoja iliyopo mezani.
Alisema kitendo cha kupoteza muda kuzungumzia
suala la kuchezewa kwa saini halitakiwi kwani kama maudhui yake hayakuchezewa
basi hoja ya muundo wa Muungano uamuliwe na wananchi wenyewe.
“Tusianze kupoteza muda kwa mambo ambayo
hayapo cha msingi wananchi wenyewe waulizwe wanaupenda Muungano au la lakini
tusianze kumtafuta mchawi kuwa saini zimechezewa wananchi waamue wenyewe kuhusu
Muungano,” alisema Mwakagenda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MSEKWA:SITTA ANA LAKE JAMBO.”
Post a Comment