Monday, April 7, 2014
RWANDA YAKUMBUKA MAUAJI YA KIMBARI.
Do you like this story?
Rwanda inaadhimisha miaka 20 tangu kutokea
mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Watu laki nane waliuawa wengi wakiwa wa
kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri. Wote waliuawa na watutsi
wenye msimamo mkali.
Hii leo Rais Paul Kagame anatarajiwa kuwasha
mwenge ambao utasalia hivyo kwa siku 100 , kipindi ambacho mauaji ya kimbare
yalifanyika.
Mgogoro wa kidiplomasia umesababisha Waziri
wa sheria wa Ufaransa, kujiondoa katika shughuli za kumbukumbu ingawa Ufaransa
inasema kuwa balozi wake ataiwakilisha nchi hiyo.
Wengi wa waathiriwa wa mauaji ya Rwanda,
walishambuliwa kwa mapanga kwa siku 100. Mauaji hayo yalianza Aprili mwaka
1994, punde baada ya kufariki kwa hayati Rais Juvenal Habyarimana
Alifariki wakati ndege yake iliposhambuliwa
katika anga ya Kigali na kudunguliwa.
Baadhi ya viongozi wa kidini walihusishwa na
ghasia zilizofuata kifo cha Habyarmana.
Mauaji ya kimbari yaliisha mwezi Julai 1994
wakati chama cha RPF, kilichokuwa cha waasi wa Tutsi wakati huo, kilipoingia
nchini humo kutoka Uganda na kuchukua uongozi wa nchi hiyo.
Kumbukumbu zinaanza kwa kuwekwa mauwa katika
eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo na kufuatiwa na kuwashwa kwa mwenge katika
uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali.
Mwenge huo umekuwa ukitembezwa katika nchi
hiyo kwa miezi mitatu iliyopita
Viongozi wa kimataifa akiwemo waziri mkuu wa
zamani wa Uingereza Tony Blair,aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na
katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Mnamo Jumapili mamia ya watu walihudhuria
maombi kuwakumbuka maelfu waliouawa .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RWANDA YAKUMBUKA MAUAJI YA KIMBARI.”
Post a Comment