Wednesday, April 16, 2014
TANESCO MBEYA YAMKAMATA MWIZI WA UMEME.
Do you like this story?
Mkuu wa usalama wa TANESCO Mkoa wa Mbeya. |
Huyu ndiye Mtuhumiwa |
Hii ndio Sehemu aliyokuwa akiiba Umeme katika mita ya Ruku |
Shirika la
Umeme Tanesco Mkoani Mbeya bado linakabiliwa na Tatizo la kuwepo kwa mafundi
umeme feki wa mitaani ambao wamekuwa wakiunganishia wananchi huduma hiyo hali
ambayo imelifanya shirika hilo kuingia hasara kubwa.
Hatua hiyo
inakuja kufuatia kuwepo kwa msako unafanywa na shirika hilo Mkoani Mbeya na
maeneo mengine kwa ujumla lengo la
kubaini watu wanaolihujumu shirika hilo.
Afisa
Usalama mwandamizi wa shirika hilo kwa Mkoa wa Mbeya Ndugu Siprian Lugazia
amesema vitendo vya kuliibia shirika kwa kujiungnishia umeme majumbani vimeanza
kuibuka upya katika kipindi cha kuanzia mwezi January hadi Aprily kwa baadhi ya
maeneo mkoani humo.
Amesema
wamekuwa wakipata taarifa mbalimbali toka kwa baadhi nya wananchi juu ya kuwepo
kwa vitendo hivyo.
Amesema mara
baada ya kufuatilia taarifa hizo walibaini kuwepo kwa hali hiyo kwa baadhi ya
wateja wao ambao hata hivyo baadhii yao walikili kufanya udanganyifu huo huku baadhi yao
wakidai kuunganishiwa na mafundi wa mitaani .
Hata hivyo
amefafanua kuwa hivi karibuni wamekamata mmoja wa wajasilimali wawanaojihusisha
na uchomeleaji katika eneo la Ilomba jijini mbeya na kumchukulia hatua za
kisheria
Hata hivyo
Afisa huyo amesema msako huo utaendelea kufanyika mara kwa mara kwa lengo la
kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TANESCO MBEYA YAMKAMATA MWIZI WA UMEME.”
Post a Comment