Tuesday, April 8, 2014
WANAFUNZI 2,006 WALIOFAULU, BADO HAWAJARIPOTI SHULENI MKOANI SINGIDA
Do you like this story?
Na Nathaniel
Limu, Singida
JUMLA ya
wanafunzi 2,006 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu mkoani
hapa bado hawajaripoti katika shule walizopangiwa.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Afisa Kazi Sekretariati mkoani Singida,Jacob Elias
wakati akitoa taarifa ya usajili wa wanafunzi kidato cha kwanza mwaka huu mbele
ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa
mkutano wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mjini Singida.
Amesema
wanafunzi hao ambao bado hawajaripoti hadi sasa ni sawa na asilimia 19 ya
wanafunzi wote 10,802 waliofaulu mtihani wa taifa wa kumaliza shule za msingi.
Akifafanua,Jacob
amesema wilaya ya Manyoni inaongoza kwa wanafunzi 585 ambao hawajaripoti kuanza
kidato cha kwanza hadi sasa.
“Manyoni
inafuatiwa na Wilaya ya Ikungi ambayo wanafunzi 503 hawajaripoti kuanza kidato
cha kwanza hadi sasa.Iramba 318, Manispaa ya Singida 270, Singida vijijini 238
na Mkalama 92″, amesema Jacob.
Amesema kila
Halmashauri na Manispaa zinapaswa kuweka mikakati bora na sahihi ili
kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu, ajulikane yupo wapi aweze kufuatiliwa
na kuanza masomo.
Kuhusu ajira
ya walimu wapya,Jacob amesema mkoa umepangiwa walimu wapya 469 nwa shule za
msingi na 636 wa shule za sekondari.
“Kwa upande
wa walimu hao wapya wa sekondari,sanaa imepangiwa walimu 129 wenye diploma na
418 wenye digrii.Sayansi wenye diploma ni 36 na digrii 53″,amesema.
Jacob amesema
kutokana na mchanganuo huo, walimu wa sayansi na hisabati ni 89 na hili bado ni
janga kubwa kwa mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.
Amesema
walimu hao wachache,watumiwe kikamilifu ili waweze kuzalisha wanasayansi wengi
watakaopelekea kupata walimu wa kutosha wa sayansi kimkoa na kitaifa kwa
ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI 2,006 WALIOFAULU, BADO HAWAJARIPOTI SHULENI MKOANI SINGIDA”
Post a Comment