Tuesday, April 8, 2014
MTO KIKAMBA UMEKUWA TISHIO KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA UDINDE CHUNYA.
Do you like this story?
Picha na Fahari News
Wakazi wa
kijiji Cha Udinde Kata ya Kapalala Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wameiomba
serikali kuwajengea Daraja katika Mto Kikamba ambao umekuwa ukihatarisha maisha
yao kwa kuwa na mamba wengi.
Wakizungumza
na Fahari News blog baadhi ya wananchi hao wamebainisha kuwa mto huo umekuwa
ukihatalisha maisha yao kwa muda mrefu hasa katika kipindi cha mvua ambapo maji
hufurika hivyo kusababisha mamba kuzagaa ovyo.
Wamesema,
mamba hao wamekuwa wakileta madhara kwa binadamu kwani hivi karibuni mwanamke
mmoja Yulita Sipiliano(54) mkazi wa Kijiji cha manda chini karibu na Ziwa
Rukwa amepoteza maisha baada ya kutafunwa na mamba.
Sisi
tunaiomba serikali itujengee daraja katika mto huu kwani watu wamekuwa
wakitumia mitumbwi kuvuka ambayo ni hatari kwa maisha ya watu hususani
wanafunzi,”amesema Alex Martin mkazi wa Kijiji cha Udinde.
Amesema,
pia wakinamama wajawazito wamekuwa wakijifungulia njiani kutokana na
kuchelewa kupata huduma ya usafiri ambayo kwa asilimia kubwa imekuwa
ikitolewa na waendesha mitumbwi.
“Wanawake
wajawazito wanapata tabu sana hasa nyakati za usiku kwani waendesha mitumbwi
wengi wamekuwa wamelala hivyo baadhi yao hujikuta wakipoteza maisha
pamoja na watoto wao,”amesema.
Kufuatia
hali hiyo ameiomba serikali kuhakikisha inafanya mpango wa haraka katika
kumaliza changamoto hiyo kwani daraja hilo ndio mkombozi kwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTO KIKAMBA UMEKUWA TISHIO KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA UDINDE CHUNYA.”
Post a Comment