Sunday, March 5, 2017
MAKONDA AWARUHUSU WATU WAENDELEE KUMSEMA MITANDAONI KWA KUWA WATANYAMAZA TU
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio
katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa
mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.
Amesema, mapambano dhidi ya dawa za
kulevya ni ya kufa au kupona.
“Mfahamu kuwa tunapambana
kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema
kwamba tunaendelea kunyooka,”amesema
Makonda.
Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa
anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo
lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.
“Huwezi kufanya kazi ya
kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya
kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.
Amesema katika kipindi hicho ambacho
amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele
zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya
chuma kilichonyooka ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa
imenyooka.
Amesema kelele hizo zitapita na mwisho
lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa
lililojengwa na uchumi imara.
Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa
jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi
sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.
“Nitoe pongezi kwa Jeshi la
Polisi dawa za kulevya zimepungua sasa Dar es Salaam na pia niwapongeze pia
vijana ambao wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.
Aliwaasa wananchi kushirikiana na Rais
John Magufuli ambaye anafanya jitihada kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora.
Kuhusu Kigamboni alisema anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao
haujaharibiwa na matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana
walioharibika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na
vijana wachapakazi.
“Watu watakapokuja
Kigamboni wakute ni mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio
salama usio na uhalifu,”amesema
Makonda.
Amewataka wakazi wa wilaya hiyo
kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na viongozi wake katika
kutimiza ndoto hiyo ya kuifanya Kigamboni tulivu na salama.
Amewaasa wazazi kuhakikisha
wanafuatilia mienendo ya watoto wao kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya
dawa za kulevya na pia vijana kuchungana wao wenyewe.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema
lengo la tamasha hilo ni kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo,
kuwakutanisha vijana kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali
katika kufanya mazoezi.
Tamasha hilolilihudhuriwa pia na Mbunge
wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel
Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
A
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAKONDA AWARUHUSU WATU WAENDELEE KUMSEMA MITANDAONI KWA KUWA WATANYAMAZA TU”
Post a Comment