Sunday, March 5, 2017
GAZETI LA MAWIO LAIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI.KUREJEA MTAANI TENA
Do you like this story?
HATIMAYE gazeti la MAWIO lililofutwa na
serikali ya Tanzania na kuacha kuchapishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, limerejea
mtaani kwa uamuzi wa Mahakama Kuu.
Serikali ililifuta gazeti hilo na kulizuia kuchapishwa kwa njia yoyote ile
Januari 15, mwaka jana- 2016.
Uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa Jumanne ya
wiki hii, umetupilia mbali amri ya serikali ya “kuliua na kulizika kabisa”
gazeti hilo lililokuwa likitoka kila wiki – Siku ya Alhamisi.
Mahakaka Kuu ilisema kuwa amri ya serikali kuliua MAWIO
haikuwa sahihi, hivyo “gazeti hilo lilionewa.”
Jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji
Sakieti Kihiyo, limesema gazeti la MAWIO halikupewa nafasi ya kujitetea kabla
ya hatua ya serikali ya kulifuta kutoka orodha ya msajili wa magazeti nchini.
Msajili wa magazeti nchini ni Idara ya
Habari Tanzania (MAELEZO).
Jaji Ignas Kitusi ndiye alisoma uamuzi wa
Mahakama kuu – kwa niaba ya jopo siku ya Jumanne, wiki iliyopita (Februari 28).
Jaji mwingine aliyekuwa kwenye jopo hilo, ni Jaji Ama-Isario Munisi.
Serikali ililifuta gazeti la MAWIO tarehe 15
Januari 2016 baada ya kudaiwa kuandika ilichoita habari na makala za
“kichochezi.”
Utawala wa Kampuni ya Victoria Media
Services Limited, wachapishaji wa gazeti la MAWIO, uliamua kufungua kesi
mahakamani. Hii ni kesi Na. 15 ya mwaka 2016.
Wakili wa MAWIO, Dk. Rugemeleza Nshalla, kuwa
hatua ya serikali iliegemea falsafa ya “…Nyonga kwanza na sikiliza baadaye.”
Dk. Nshalla amesema katika mazingira yoyote
yale, sharti walalamikiwa wapate nafasi ya kujieleza na kusiklilizwa na
mahakama kwanza kabla ya hukumu kutolewa.
lilimpata Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri
Mkuu wa gazeti la MAWIO, Simon Mkina ambaye amesema alishangazwa sana na hatua
ya serikali kufuta alichoita “mdomo wa wananchi.”
“Kufuta chombo hiki au kingine kama hiki, ni
kukiri kuwa serikali haipendi kusikia kutoka kwa wananchi…” amesema Mkina
Mkina amesema MAWIO limekuwa gazeti
linalozingatia maadili na kufuata weledi wa hali ya juu katika kuandika na
kuchapisha habari na makala na kuongeza kuwa limekuwa gazeti pekee linalotoa
uwanja mpana kwa wananchi kuandika mawazo yao ili kuchochea uwajibikaji wa
viongozi wa serikali.
Mkina amesema kufuatia uamuzi huo wa
Mahakama Kuu, MAWIO litarejea mtaani Alhamisi ya wiki hii na kuahidi kuwapa
wasomaji wake habari zilizofanyiwa kazi ya ziada.
“Kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja, wakati
gazeti halipo mtaani – likiwa limefutwa na serikali, pamoja na kupoteza ajira
za watu na kuingia katika hasara kubwa, bado tulikuwa na kazi ya kujiuliza ni
wapi tulikosea na je, lini tutapewa haki yetu? Bahati nzuri haki yetu imefika,”
aliongeza Mkina akiongea.
Uamuzi na hatua ya kulifuta MAWIO,
lililokuwa likichapishwa kila Alhamisi, ulitangazwa na Nape Nnauye, Waziri wa habari, vijana,
utamaduni, sanaa na michezo.
Tangazo lililotolewa katika gazeti la
serikali, Na. 55 la Januari 15, 2016, lilisema serikali inachukua uamuzi wa
kulifuta kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo kupitia Sheria ya Magazeti ya 1976;
sura ya 229 kifungu cha 25(1).
Chanzo: Fikrapevu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ GAZETI LA MAWIO LAIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI.KUREJEA MTAANI TENA”
Post a Comment