Thursday, March 2, 2017
MREMBO AJITANGAZA KUWA ANAISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI
Do you like this story?
Saidy Brown ni raia wa Afrika Kusini, alizaliwa akiwa na Virusi Vya UKIMWI lakini alijua akiwa na umri wa miaka 14
“Nilipogundua kuwa nina Virusi Vya
UKIMWI nikiwa na miaka 14, sikuwa na hakika nitaishi hadi kufika miaka
18, lakini nitatimiza miaka 22 mwaka huu.”
Tangu msichana Saidy Brown aweke ujumbe
huo kwenye ukurasa wake wa twitter Ijumaa iliyopita, maelfu ya watu
wameusambaza ujumbe huo wenye kuonesha matumaini, wengi wao wakimsifu
kwa ujasiri wake wa kuongea mbele ya kadamnasi kuhusu ufahamu wake juu
ya Virusi Vya Ukimwi.
Dada huyu mwanaharakati Saidy,
anayejielezea kama mshindi katika harakati za kuelimishwa kuhusu Virusi
Vya UKIMWI na UKIMWI, ameongea na kituo cha utangazaji cha nchini
Uingereza, BBC kuhusu mrejesho wa kipekee aliopata kutoka kwa watu baada
ya kuweka ujumbe huo kwenye mtandao wa kijamii, kwanini ilichukua muda
mrefu kwake kugundulika kuwa na virusi na changamoto za kuwa katika
mahusiano ya kimapenzi na mtu mwenye Virusi Vya UKIMWI.
Uamuzi wa kuandika kwenye mtandao wa kijamii
“Muda wote nimekuwa wazi kuhusu hali yangu ya kiafya. Nilianza kujitangaza nikiwa na miaka 18. Mara nyingi natumia mtandao wa Facebook kuongea na watu kuhusu Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI,” amesema.

“Lakini nimekuwa nikipata msukumo wa
kuandika kwenye mtandao wa Twitter pia ili isiwe ninaishia kwenye
marafiki zangu wa Facebook peke yake. Nilihitaji dunia nzima izungumzie
Virusi hivi.”
Kuendeleza mjadala
“Muitikio wa watu umekuwa mkubwa. Kuna watu wamenifata na kunieleza kuhusu maisha yao, na nimefurahishwa na hilo. Napenda kuanzisha mijadala kuhusu Virusi Vya UKIMWI. Siamini kabisa kuichukia kama jambo lisilotakiwa kuzungumzwa. Nataka tulizungumzie, sababu tukishaliongelea sana basi itakuwa rahisi kwetu kupambana na dhana potofu zinazohusishwa nao.

“Kuna watu wanachojua wao ni kusema
“hapana” tu kuhusu mijadala inayohusiana na UKIMWI lakini sina haja ya
kuwajibu. Nawaacha tu. Nilipokuwa mdogo nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu
watu watakavyoniangalia baada ya kujitangaza. Lakini sasa nimekuwa na
maoni ya watu hayaniathiri kabisa. Nadhani nimekuwa imara zaidi kihisia
sasa. Siku hizi nikijibiwa vibaya hainiumizi kabisa.”
Kuishi na Virusi Vya UKIMWI
“Sijawahi kunyanyapaliwa au kutengwa. Naweza kusema kuwa nilikuwa najitenga mimi mwenyewe toka nikiwa na miaka 14 mpaka nilipofikisha miaka 18, kwa sababu sikutaka kuzungumzia hali yangu ya kiafya. Ni familia yangu tu ndio ilikuwa inajua, hakuna mtu mwengine zaidi yao. Nilipofikisha miaka 18 niliamua kuanza kujitangaza. Nakiri kuwa huu umekuwa uamuzi bora na wa busara.

“Ninapotoka, nimekuwa mtu wa kwanza kabisa kuwahi kujitangaza kuhusu hali yangu kama nilivyofanya.
“Lakini muitikio wa watu pamoja na kupewa moyo ni kwa kiwango kikubwa kwa sababu iwe ni kwangu au kwa mtu mwengine, ukweli ni kwamba watu wanaishi na Virusi Vya UKIMWI – haijalishi tukiamua kuviongelea au kuwa kimya.”

Jinsi alivyogundua
“Nilipokuwa na miaka 14, nilikwenda kwenye tamasha la siku ya vijana kuiwakilisha shule yangu. Kwenye tamasha hilo kulikuwa na wataalamu waliokuwa wanapima Virusi Vya UKIMWI, ushauri nasaha na mambo ya namna hiyo.

“Tulipofika tuliulizwa kama tungependa kupima afya zetu. Nilikuwa miongoni mwa tuliopimwa.
“Nilishangaa, sikuamini kabisa. Nilikuwa na miaka 14 tu wakati huo kwahiyo nikawa najiuliza: ‘Kivipi? Nina miaka 14 tu… sijawahi kufanya chochote. Inawezekana vipi?’

“Niliporudi nyumbani nikamwambia
shangazi yangu na yeye ndiye aliniambia kuwa nilizaliwa nikiwa na virusi
hivyo. Wazazi wangu walifariki kutokana na magonjwa yanayoambatana na
UKIMWI, ambayo sikuwahi kuyajua. Mama yangu alifariki nikiwa na miaka
10, baba nikiwa na miaka tisa.”
Mahusiano ya kimapenzi
“Kwa sasa nipo kwenye mahusiano. Inanifurahisha sana kwakuwa huwa naelezea hali yangu ya kiafya mwanzo wa mahusiano yangu.
“Kwahiyo kama mtu akiamua kubaki na mimi basi inakuwa vizuri, na kama akiamua kuondoka, ni vizuri pia.

“Siwezi kuwachukia kwa sababu watu bado
wana kasumba zao kuhusu Virusi Vya UKIMWI. Huwa simlaumu mtu anayesema:
‘Siwezi kuishi na wewe kwa sababu una virusi’.
Nilishawahi kuambiwa hivyo kipindi cha
nyuma, iliniumiza sana. Lakini baada ya muda walirudi na kuniomba
msamaha. Kwa sasa tunaongea tu, hatuna matatizo, nimeshawasamehe.”
Ninajali afya yangu
“Kwakweli mimi huwa siangalii sana nakula kitu gani, lakini nahakikisha kuwa nakunywa dawa zangu kwa muda sahihi kila usiku. Hakuna siku ninayoacha.

Ndoto za kuwa na familia
Saidy amesema kuwa anategemea atakuwa na familia hapo baadae na amekuwa akijifunza mbinu za kukabiliana na maambukizi kutoka kwake kwenda kwa mwenza wake au mtoto.
“Mimi nilipata maambukizi kutoka kwa mama-kwenda kwa mtoto, kwahiyo sitataka kuwafanya watoto wangu wapate maambukizi kama ilivyokuwa kwangu,” amesema.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MREMBO AJITANGAZA KUWA ANAISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI”
Post a Comment