Sunday, March 5, 2017
HAWA NDIO WABUNGE TISA WALIOCHAGULIWA NA RAIS DKT MAGUFULI
Do you like this story?
Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 66- 1 (a)-(e) inataja ina tano za
wabunge watakaounda Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika
ibara hiyo ya 66, kifungu cha (e) kinampa mamlaka Rais wa Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania kuteua wabunge wasiozidi 10 ambapo kati hao, wasiopingua watano
wanatakiwa kuwa wanawake. Ibara hiyo inasomeka “Wabunge wasiozidi kumi
walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya
67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b).”
Hadi
sasa Rais Dkt Magufuli ameteua wabunge 9 huku akiwa amebakisha nafasi 1
kukamilisha mamlaka aliyopewa na katiba. Wabunge hao walioteuliwa hadi sasa ni
pamoja na;-
1.
Dk.
Tulia Ackson Mwansasu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2.
Prof.
Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
3.
Prof.
Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
4.
Dk.
Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
5.
Dk.
Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango.
6.
Anne
Kilango Malecela.
7.
Prof.
Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.
8.
Alhaji
Abdallah Bulembo, na
9.
Salma
Kikwete
Awali,
Rais Dkt Magufuli alikuwa amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa mbunge
lakini alijiuzulu wadhifa huo baada ya kuteuliwa kuwa Balozi.
Hadi
sasa Rais Dkt Magufuli ameteua wabunge wanaume watano na wabunge wanawake
wanawake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 Responses to “HAWA NDIO WABUNGE TISA WALIOCHAGULIWA NA RAIS DKT MAGUFULI”
March 5, 2017 at 11:47 PM
PAMOJA Sanahttps://laelayetu.blogspot.com/
Post a Comment