Monday, March 6, 2017

RAISI WA CHEMBA YA BIASHARA, VIWANDA NA KILIMO AHIMIZA WATANZANIA KUTUMIA FURSA YA SOKO LA AWALI.



 

Rais wa  TCCIA, Ndibalema John Mayanja (katikati), akizungumza hii leo Jijini Mwanza kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa biashara. Kulia ni Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leo

 Rais  wa Chemba ya Biashara,viwanda na kilimo, Ndibalema Mayanja, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mikoa ya Mwanza na Kagera kuchangamkia soko la awali la hisa za TCCIA Investment PLC.

Raisi wa TCCIA Ndibalema John Mayanja akizungumza na wafanyabiashara waliohudhuria kwenye mkutano  huo mkoani Kagera


Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa mikoa hiyo bwana Mayanja  alisema “TCCIA Investment PLC ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja, imara na inafanya vizuri sana kwani tangu ianzishwe mwaka 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97 imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 na imekuwa ikilipa gawiwo kwa wanahisa wake. Hii ni fursa muhimu na adhimu muitumie kabla ya tar 14 mwezi huu March. “ alisema Mayanga
Raisi huyo wa Chemba akiwa ziarani mkoani Mwanzan na Kagera pia alifanya kazi ya kujenga uhai wa chemba kwa kukutana na viongozi mbalimbali katika mikoa hiyo.

Baadhi ya wafanyabiashara na wakzi wa Mkoani  Kagera waliohudhuria kwenye mkutano huo

Mshauri TCCIA Mkoani Mwanza Lazzaro akitoa neno la shukrani kabla ya mkutano kuanza, kulia ni Raisi wa TCCIA Ndibalema Mayanja

 

 

0 Responses to “RAISI WA CHEMBA YA BIASHARA, VIWANDA NA KILIMO AHIMIZA WATANZANIA KUTUMIA FURSA YA SOKO LA AWALI.”

Post a Comment

More to Read