Sunday, March 5, 2017

HAWA NDIO WABUNGE TISA WALIOCHAGULIWA NA RAIS DKT MAGUFULI




Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 66- 1 (a)-(e) inataja ina tano za wabunge watakaounda Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ibara hiyo ya 66, kifungu cha (e) kinampa mamlaka Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuteua wabunge wasiozidi 10 ambapo kati hao, wasiopingua watano wanatakiwa kuwa wanawake. Ibara hiyo inasomeka “Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b).”

Hadi sasa Rais Dkt Magufuli ameteua wabunge 9 huku akiwa amebakisha nafasi 1 kukamilisha mamlaka aliyopewa na katiba. Wabunge hao walioteuliwa hadi sasa ni pamoja na;-
1.   Dk. Tulia Ackson Mwansasu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.   Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

3.   Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

4.   Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

5.   Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango.
6.   Anne Kilango Malecela.

7.   Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.
8.   Alhaji Abdallah Bulembo, na

9.   Salma Kikwete

Awali, Rais Dkt Magufuli alikuwa amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa mbunge lakini alijiuzulu wadhifa huo baada ya kuteuliwa kuwa Balozi.

Hadi sasa Rais Dkt Magufuli ameteua wabunge wanaume watano na wabunge wanawake wanawake.

1 Responses to “HAWA NDIO WABUNGE TISA WALIOCHAGULIWA NA RAIS DKT MAGUFULI”

Ombeni Utembele said...
March 5, 2017 at 11:47 PM

PAMOJA Sanahttps://laelayetu.blogspot.com/


Post a Comment

More to Read