Tuesday, April 8, 2014
MBWA WALIOMLA MTOTO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE NUSURA WAMLE BABA MTU.
Do you like this story?
ZIMEKATIKA wiki mbili tangu kuzikwa kwa
mtoto Christian Alex (6) aliyeuawa kwa kushambuliwa na mbwa watatu
waliodaiwa ni wa Ubalozi wa Qatar nchini, mbwa hao wamemkosakosa baba mtu.
Tukio la kuuawa kwa mtoto huyo lilijiri Kunduchi Jangwani Beach jijini Dar Machi 26, mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo, mara baada ya
kumaliza shughuli ya kumzika marehemu katika Makaburi ya Mburahati jijini Dar,
baba mzazi Alex Augustino alikaa kikao na ndugu ili kuangalia uwezekano wa
kufika kwenye makazi hayo ya ubalozi na kuzungumza nao kujua hatima ya sakata
hilo.
Baada ya makubaliano, familia hiyo
ilielekea kwenye makazi hayo ambapo wengine walifikia nje kwanza, Alex
aliingia ndani kucheki usalama, yaani kama mbwa hao walikuwa eneo hilo au la!
Kabla wengine hawajaingia.
“Kabla Alex hajamaliza kukagua, mbwa
hao walimtoa mkuku. Ilikuwa na yeye ashambuliwe, ikabidi aruke ukuta ili
kutoka nje.
“Kitendo hicho kilimtia uchungu bibi wa
marehemu, yaani mama wa Alex aliyekuwa kwenye gari ambapo alishindwa kuvumilia
na kuangua kilio.
“Safari ya kuwaona wahusika wa ubalozi
iliishia hapo. Wote walirudi nyumbani,” kilisema chanzo.
Chanzo chetu kiliendelea kudai kuwa baada ya kukaa kwa siku kadhaa, baba huyo wa marehemu alipigiwa simu na bosi wake akitakiwa kurudi kwani bado alitakiwa kuendelea kuishi mahali hapo akiwa msimamizi wa nyumba.
Habari zinadai kwamba, katika hali
isiyokuwa ya kawaida, alipofika nyumbani hapo hakukuta mbwa hata mmoja.
Mpaka tunakwenda mitamboni balozi huyo
hakupatikana lakini familia nayo inasisitiza kwamba wanataka kukutana na
viongozi wa ubalozi na kujadili ni kitu gani kitaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBWA WALIOMLA MTOTO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE NUSURA WAMLE BABA MTU.”
Post a Comment