Monday, May 26, 2014

KANDORO ATULIZA HASIRA ZA WANANCHI MARA BAADA YA KUFUNGA BARABARA KWA MASAA KADHAA



Wananchi wakiwa barabarani huku wakiwa wamepanga magogo kushinikiza kuonana na mkuu wa mkoa wa mbeya mara baada ya mwananchi mwenzao kugongwa na kufa papo hapo


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza kwa msisitizo na wananchi hao


Mwili wa Marehemu ukiwa chini pembezo mwa Barabara


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi baada ya kuzungumza kwa kuwasihi wananchi hao kutotumia sheria mkononi(Picha na fahari news)


WANANCHI wa kijiji cha  Nanyala Wilayani Mbozi, leo wamefunga barabara  kuu ya  Tanzania- Zambia  zaidi ya masaa matano na kusababisha kukwama kwa wasafiri waendeo nchi za kusini mwa Afrika na jijini Dar es Salaam.

Wananchi hao ambao waliamua kutumia maiti ya mtoto wa miaka mitano Alfani Dumu ambaye aligongwa na gari ndogo ya abiria (HICE) kwa kuilaza barabarani hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa njia hiyo.

Wakizungumza  kwenye eneo la tukio, walisema tukio hilo limetokea majira ya saa tatu za asubuhi mara baada ya marehemu mtoto huyo akiwa anavuka barabara akitokea shuleni  kugongwa na gari hilo.

Akielezea sababu ya wao kufunga barabara hiyo, Mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka kutaja jina lake  amesema wamechoshwa na ahadi hewa za serikali kwa kushindwa kuwatekelezea ombi lao  la kuiweka barabara hiyo matuta, alama za  barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani ambaye atakuwa na tochi.

Amesema Zaidi ya miaka mitatu wamekuwa wakipigia kelele suala hilo lakini hakuna utekelezaji wa aina yoyote uliofanyika .
tumeiomba serikali kuangalia uwezekano wa eneo hili la barabara

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, amewataka wakazi hao kuondoa maiti hiyo kisha kufungua njia ili watumiaji waweze kuitumia kwani suala lao amelipokea na kwamba atalifanyia kazi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo kuhakikisha linaweka askari wa usalama barabara kwa muda wote katika eneo hilo pamoja na kuhakikisha kuwa askari hao wanakuwa na vifaa vya kupimia mwendo kasi.

Amesema kwa dereva yoyote atakaye kwenda kinyume na taratibu ameagiza kuchukuliwa kwa  hatua kali kwa lengo la kukomesha vitendo hivyo.

Aidha, Kandoro amemuagiza Wakala wa barabara  nchini(TANROAD) Mkoa wa Mbeya, kulifanyia matengenezo eneo hilo kwa kuweka matuta pamoja na alama za barabarani mapema kesho badala ya kuchukua muda mrefu.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, aliwahakikishia usalama wakazi hao na kwamba askari wa tochi watakuwa kwenye eneo hilo huku akiwasisistiza kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi mara vitendo vya  uhalifu vinapotokea.

Hata hivyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzungumza na wananchi haio na kuwasihi kufungua barabara hiyo mara moja wananchi hao walitii agizo hilo na usafiri kuendelea kama kawaida majira ya saa3 jioni.


0 Responses to “KANDORO ATULIZA HASIRA ZA WANANCHI MARA BAADA YA KUFUNGA BARABARA KWA MASAA KADHAA ”

Post a Comment

More to Read