Tuesday, May 20, 2014
MBEYA CITY FC YAENDELEA KUJIWINDA NA CECAFA NILE BASIN CUP JIJINI DAR
Do you like this story?
WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya
City fc bado ipo jijini Dar es salaam kujiandaa na safari ya kwenda Sudan
kushiriki michuano mipya ya CECAFA Nile Basin inayotarajia kuanza mei 22 mpaka
juni 4 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka
Mwalwisyi ameuambia mtandao huu kuwa asubuhi hii wanaendelea na mazoezi katika
uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.
“Ninavyozungumza na wewe muda huu tupo
hapa Karume. Tunaendelea vizuri na mazoezi yetu. Na mambo yakikaa sawa muda
wowote tutaanza safari ya kwenda Sudan”. Alisema Mwalwisyi.
Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji
wote wapo katika morali kubwa na wanahamu kubwa ya kwenda kushiriki michuano
hii mikubwa.
“Wachezaji wetu siku zote wanapenda
kucheza. Hii ni nafsi nyingine nzuri ya kupata uzoefu wa michuano ya kimataifa.
Najua itakuwa changamoto kwetu, lakini tutapambana kwa kila mechi”.
“Sisi bado ni wachanga katika soka.
Michuano kama hii ni msingi mzuri kwetu”
“ Tutaitumia vyema nafasi hii
kuhakikisha tunafanya vizuri, tumekuwa tukitumia muda mwingi kuwapa mbinu za kimpira wachezaji wetu”. Aliongeza
Mwalwisyi.
Mwalwisyi aliwaomba mashabiki wao na
watanzania wote kuwaombea mafanikio katika mashindano hayo kwasababu kufanya
vizuri itakuwa sifa kwa taifa zima.
Mbeya
City fc waliopo kundi B wataanza kampeni zao mei 23 kwa kukabiliana na El
Merreikh Al Fasher .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CITY FC YAENDELEA KUJIWINDA NA CECAFA NILE BASIN CUP JIJINI DAR”
Post a Comment