Monday, May 19, 2014
MENEJA EWURA AJIUA HOTELINI BAADA YA KUOJIWA NABUNGE
Do you like this story?
Meneja
Biashara wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) amekutwa
amekufa hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili
jijini Dar es Salaam akitoka Dodoma ambako alihojiwa na Kamati ya Bunge ya
Bajeti.
Meneja
huyo, Julius Gashaza, ambaye alikuwa na jukumu la kupanga bei za mafuta za kila
mwezi, alihudhuria kikao hicho mjini Dodoma kwa siku mbili; Ijumaa na Jumamosi
iliyopita kuhusu mambo mbalimbali, yakiwamo kiwango cha mafuta kinachoingizwa
nchini, mgawo wa fedha unaotolewa na Ewura kwenda kuhudumia umeme vijijini
(Rea) na fedha za mfuko wa barabara.
Jeshi
la Polisi, Mkoa wa Temeke limethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa meneja huyo
alikutwa amejinyonga kwa kutumia tai kwenye hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo
Yombo Vituka wilayani Temeke.
Nyumbani
kwa meneja huyo wa Ewura, kulikuwa na waombolezaji waliokuwa kwenye vikundi na
kikao cha maandalizi ya mazishi kilifanyika ndani ya nyumba ya marehemu iliyopo
Yombo Vituka na baadaye kuhamia nyumba ya jirani.
Kamati
ya Bunge ya Bajeti, inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge,
ilikutana na maofisa wa Ewura, akiwamo Gashaza na wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na kugundua kuwapo kwa tofauti katika takwimu za kiwango cha mafuta
kilichostahili kutozwa kodi.
Gashaza
alikwenda Dodoma kutoa ripoti ya Ewura kwenye kamati hiyo ya Bunge
akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo, takwimu za Ewura ziliashiria
kuwa fedha zilizopatikana ni nyingi zaidi ya zile zilizoelezwa na TRA, lakini
Wizara ya Fedha ilisisitiza zifuatwe takwimu za mamlaka ya mapato.
Habari
hizo, zinasema baada ya kurejea Dar es Salaam juzi majira ya saa tatu usiku,
Gashaza hakwenda nyumbani kwake na badala yake alikwenda kwenye hoteli iliyo
karibu na nyumbani ambako mkewe na ndugu yake mmoja walimfuata na akawaeleza
kuwa anahisi kutishiwa maisha yake.
Baadaye
walifanya maombi maalumu kabla ya kuachana naye.
Inadaiwa
kuwa marehemu aliomba akalale hotelini kwa sababu hakuona kama ana amani kulala
nyumbani kwake na ilipofika asubuhi alikutwa ‘amejinyonga’ ndani ya chumba
alicholala hotelini humo.
Nyumbani
kwa marehemu waombolezaji walikusanyika katika makundi, lakini baada ya kukaa
katika kikao cha familia walitoka na kauli moja kuwa hawatasema chochote na
kwamba jukumu hilo libaki mikononi kwa polisi.
Polisi wathibitisha.Chanzo Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MENEJA EWURA AJIUA HOTELINI BAADA YA KUOJIWA NABUNGE”
Post a Comment