LOUIS van
Gaal anatarajia kumteua mshambuliaji wake hatari Robin van Persie kuwa
nahodha wa kikosi chake mara atakapojiunga na Manchester United baada ya
kumalizika kwa kombe la dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Jumamosi
iliyopita Van Persia aliifungia bao muhimu timu ya taifa ya Uholanzi katika
mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador na kulazmisha sare ya 1-1.
Van Gaal
amekuwa na mahusiano mazuri na RVP ambaye ni nahodha wa timu ya taifa na sasa
anatarajia kumpa jukumu hilo katika klabu ya Man United na kumpiga chini Rooney
ambaye angekuwa nahodha wa kudumu katika utawala wa David Moyes.
Van
Persie alikuwa na majeruhi kwa muda wa wiki sita za mwishoni mwa msimu mbovu wa
Man United baada ya kuumia goti katika mechi ya UEFA dhidi ya Olympiacos mwezi
machi mwaka huu.
‘Hata kama
ametokea katika majeruhi, alifunga bao la maajabu, bao ambalo huwezi kuamini,
ni bao zuri mno,’ alisema Van Gaal baada ya mshambuliaji huyo kusawazisha
dakika ya 37 katika uwanja wa Amsterdam ArenA jumamosi.
Kwa mujibu
wa Van Gaal, kwa asimilia 100, Van Persie hayuko fiti lakini alionekana kuwa
imara na kuitendea haki pasi ya Feyenoord na kufunga bao muhimu.
‘Nilifurahishwa
na kiwango chake, pia ni nahodha wa aina yake," Alisema Van Gaal.
"Nadhani unampa mchezaji unahodha kama mna morali na falsafa
inayofanana".
"Sio
tu mambo ya uwanjani na kiwango cha mchezaji, hata maisha ya kawaida tu".
"Naamini
hilo ni muhimu sana. Naamini Van Persie na Van Gaal tuna falsafa moja".
0 Responses to “ROONEY YALA KWAKE!, VAN GAAL AMCHAGUA VAN PERSIE KUWA NAHODHA MPYA WA MANCHESTER UNITED”
Post a Comment