Monday, May 26, 2014

MGOMO WA MADEREVA NA MAKONDAKTA WA DALADALA LEO ASUBUHI KUGOMA KUPELEKA ABIRIA MWENGE KUTOKA MAKUMBUSHO, DAMU YAMWAGIKA


Kamanda wa Polisi Kinondoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea ni jinsi gani watashughulikia shida ya barabara hiyo ya kutoka kituoni makumbusho kuelekea mwenge



 Madereva na Makondakta wa mabasi yanayofanya Safari zake kati ya mbagala,tandika kupitia kituo cha makumbusho wakijadiliana na viongozi wa sumatra na polisi  Ili kuweza kujua watatoa Suluhisho gani ili kuweza kutatua tatizo la barabara mbovu eneo la makumbusho

Msururu wa daladala zikiwa ndani ya kituo cha makumbusho baada ya kugoma leo kuelekea mwenge kupeleka abiria
Hapo ni Madereva na makondakta wakilikimbiza basi la UDA ambalo lilimkata mkono dereva mwenzao wakati wanalizuia lisiweze kutoka ndani ya kituo kuendelea na safari.


 Abiria wanaotumia njia ya makumbusho kuelekea Mwenge wakitokea Tandika na Mbagala leo wameonja Joto ya jiwe kwa takribani masaa manne baada ya mabasi yanayoptumia kituo cha ndani kugoma kupeleka abiria mwenge kutokana na ubovu wa barabara za ndani wanazotumia kupita kuelekea kituo cha mwenge.

Sakata hilo lilianza pale magari yalipofika kituo cha ndani cha makumbusho na kuwashusha abiria wote na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea mwenge,ndipo mzozo mkubwa ulipozuka na kupelekea Sumatra na vyombo vya Usalama kufika eneo La Tukio na kuweza kuongea na madereva hao,lakini madereva hao na makondakta waliendelea kugoma mpaka pale walipohaidiwa kuwa ndani ya wiki moja barabara hizo zitakuwa zimerekebishwa na kuwa nzuri,hivyo watumie njia kuu kuelekea mwenge.
             PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG

0 Responses to “MGOMO WA MADEREVA NA MAKONDAKTA WA DALADALA LEO ASUBUHI KUGOMA KUPELEKA ABIRIA MWENGE KUTOKA MAKUMBUSHO, DAMU YAMWAGIKA”

Post a Comment

More to Read