Saturday, May 10, 2014

PATA MKWANJA PATA MKWANJA KAZI KWAKO KAZI KWAKO STEVE NYERERE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA WASANII UPANDE WA AMANI NJE YA BUNGE LA KATIBA.


Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amechaguliwa na Kamati ya Tanzania kwanza kuwa mwenyekiti wa wasanii wa amani ndani ya Tanzania nje ya Bunge la katiba


Steve Nyerere amesema amechaguliwa na Kamati ya Tanzania Kwanza nje ya Bunge kwa lengo la kuhamasisha Amani kwa wananchi wa Tanzania. "Walikaa kamati zao hapa Dar es salaam wakakaa Zanzibar na kura zote walizopiga zilimdondokea Steve Nyerere, mwenyekiti wa wasanii upande wa Amani nje ya Bunge la Katiba.

Baada ya hapo nilipigiwa simu ambapo nikiwa sijui lolote nilikuta kwanza barua nyumbani kwamba nahitajika kwenye kikao,nikasema ni jambo zuri, mimi naimani bila amani na mimi nilitoa ufafanuzi wangu bila amani hata kazi zangu haziwezi kwenda.

Nahitaji amani sana ili ziweze kwenda. Lakini nikasema hata wasanii bila kujali hela ya malipo, haya malipo yanakuja nchi ikiwa na amani na utulivu.Tunaona wasanii wa nchi mbalimbali duniani wanapigania amani ya za nchi zao. Kwanini sisi tushindwe,kwanini JB,Diamond,Lady Jaydee na wasanii wengine wasiwe mabalozi wa amani nchini? Tukijipanga tunaweza," amesema.

"Lakini vilevile nilichokipenda mimi nimepewa jukumu nichague wasanii wenzangu ambao wanaweza wakaitangaza amani ndani ya nchi na nje ya nchi yetu. Wapo wengi wenye uwezo kwenye ma group yote ya wasani,wapo wa filamu,muziki,ngoma za asili kote huko inabidi tupate mabalozi kumi ambao wataweza kufanya kazi kwa ukamilifu zaidi. Kwahiyo hili ni suala langu nadhani nikikaa chini nitajua nani anafaa na nani hafai".

0 Responses to “ PATA MKWANJA PATA MKWANJA KAZI KWAKO KAZI KWAKO STEVE NYERERE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA WASANII UPANDE WA AMANI NJE YA BUNGE LA KATIBA.”

Post a Comment

More to Read