Friday, May 16, 2014
POLISI WATIBUA MAANDAMANO BRAZIL.
Do you like this story?
Polisi
wa kupambana na ghasia wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya
waandamanaji katika barabara za miji ya Sao Paolo na Rio de Janeiro walipinga
mfumuko wa gharama ya uenyeji wa kombe la dunia litakaloanza mwezi ujao nchini
Brazil.
Baadhi
ya waandamanji walipura mawe na kuchoma magurudumu ya magari na kufunga
mabarabara ya miji wakidai serikali haikuzingatia matakwa ya wananchi kama vile
elimu sekta ya afya na muundo msingi .
Katika
tukio linaloibua hofu ya kuwepo kwa usalama wafanyikazi wa umma na walimu
walijiunga na waandamanaji katika miji yote mikuu ikiwemo mji mkuu wa Brasil.
Wengi
wao waliahidi kurejea mabarabarani kadri mchuano huo unavyosongea .
Mwaka
uliopita takriban watu milioni moja walishiriki maandamano wakilalamikia
ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na ongezeko la gharama ya uandalizi wa
kipute hicho cha fainali ya dimba la dunia .
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 12 June.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 12 June.
Waandamanaji
walianzia Sao Paulo,karibu na uwanja wa Corinthians Itaquera karibu na mtaa wa
Itaquera .
Uwanja
huo wa Corithians ndio utakaoandaa mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia mwaka
huu tarehe 12 juni.
Kwa
mujibu wa shirika moja la kijamii linaloandaa maandamano hayo Homeless Workers
Movement waandamanji wanaitaka serikali kutumia fedha katika ujenzi wa nyumba .
Kulingana
naye hangependa viwanja vilivyogharimu mabilioni ya dola viharibiwe ila
wafanyikazi wanaojenga viwanja hivyo wajengewe nyumba kuambatana na ubora wa
shirikisho la soka duniani FIFA.
Serikali
imepinga uhisano wowote kati ya maandamano haya na kombe la dunia .
Waziri
wa michezo Aldo rebelo amenukuliwa akisema kuwa ameona matakwa ya waandamanaji
na ikampa matumaini maandamano hayo hayataathiri ujio wa takriban watalii
milioni tatu na wageni laki sita wanaotarajiwa kuzuru miji itakayoandaa mechi
za kombe la dunia.
Hata
hivyo maandamano haya yanawadia wakati ambapo serikali inakabiliwa na mgomo wa
wafanyikazi wa umma na hata polisi katika jimbo la Pernambuco
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “POLISI WATIBUA MAANDAMANO BRAZIL.”
Post a Comment