Friday, May 16, 2014
MAN UNITED: TUMEPATA BONGE LA HASARA KWA KUVURUNDA...ILA SASA TUTASAJILI TIMU LA KUFA MTU.
Do you like this story?
Hasara: Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward (katikati) amesema klabu itakosa Pauni Milioni 30 kwa kutoshiriki michuano ya Ulaya. |
KITENDO cha
Manchester United kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kutaipa
hasara timu hiyo ya Pauni Milioni 30, imeelezwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed
Woodward.
Pamoja na hayo,
Woodward amesema kwamba haitaiathiri k;abu hiyo katika solo la
usajili. "Kutokana na mikataba ya Televisheni, tunakadiria tutakosa
Pauni Milioni 30 za michuano ya Ulaya. Matarajio ya klabu yalikuwa ni kurejea
kwenye Ligi ya Mabingwa naa utaona kwenye usajili wetu,".
Akizungumza
katika mkutano wa simu, alisema: "Katika msimu wa 2013-14, tumemaliza
vibaya katika nafasi tab saba, ambayo inamaanisha hatutashiriki michuano
ya Ulaya.
"Kuwa na
uhakika kila mmoja katika klabu anapambana kuhakikisha msimu ujao tunakuwa
katika kiwango cha juu cha Manchester United.
"Tumefanya
mabadiliko ya bench la Ufundi Aprili, tumefurahi kuwa na Ryan Giggs
kwa kumalizia msimu vizuri. Kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu katika kupata
kocha mpya na tarajia atatangazwa muda si mrefu,".
Louis van Gaal
ndiye kocha anayetarajiwa kuichukua Manchester United baada ya Fainali za Kombe
la Dunia atakapoiongoza kwa mara ya mwisho Uholanzi.
Jumatano Giggs
alitua Uholanzi na akapigwa picha na inasemakana alikwenda kufanya mazungumzo
na Van Gaal kwa niaba ya klabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAN UNITED: TUMEPATA BONGE LA HASARA KWA KUVURUNDA...ILA SASA TUTASAJILI TIMU LA KUFA MTU.”
Post a Comment