Friday, May 16, 2014
RASM SEPP BLATTER AKIRI KUFANYA MAKOSA KUWAPA QATAR UENYEJI WA KOMBE LA DUNIA 2022.
Do you like this story?
RAIS wa FIFA, Sepp Blatter amekiri kuwa
walifanya makosa kuwapa Qatar uenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka
2022.
Qatar waliwashinda wapinzani wao
Marekani, Korea kusini, Japan na Australia, lakini maamuzi ya FIFA kuwapa
nafasi ya kuhodhi michuano hiyo yalikoselewa vikali tangu yalipothibitishwa
desemba mwaka 2010.
Sababu kubwa ya watu wengi kupinga
Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia ni kwasababu ya joto kali majira ya
kiangazi ambapo kombe hilo hufanyika.
Hata hivyo FIFA walipotangaza maamuzi
yao, mwaka mmoja baada iliibuka kashfa ya rushwa ambapo ilielezwa kuwa Qatar
waliwahonga maofisa wa FIFA na kuwepa uenyeji wa fainali hizo za mwaka 2022.
Aidha, shiriki la kutetea haki za
binadamu la kimataifa limewataka FIFA kuingilia kati kwani kuna taarifa za
kunyanyaswa kwa wafanyakazi wanaojenga viwanja katika taifa hilo la Gulf.
Siku za nyuma, Blatter alikuwa anatetea
uamuzi wa FIFA kuwa ulikuwa sahihi kuwapa uenyeji Qatar, lakini kwasasa amekiri
kuwa ilikuwa makosa.
“Kiukweli yalikuwa makosa (kuwapa uenyeji
wa kombe la Dunia Qatar)”. Blatter amewaambia RTS.
“Lakini wote tunajua kuwa makosa
yanatokea katika maisha”.
“Ripoti za idara ya ufundi kutoka Qatar
zilieleza kuwa majira ya kiangazi kuna joto kali sana. Hata hivyo haikuzuia
kamati kuwapa uenyeji wa fainali za kombe la dunia, tena kwa kura nyingi”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RASM SEPP BLATTER AKIRI KUFANYA MAKOSA KUWAPA QATAR UENYEJI WA KOMBE LA DUNIA 2022.”
Post a Comment