Friday, May 16, 2014

BARCELONA HAWATASHEREHEKEA UBINGWA WA LA LIGA.....NAO ATLETICO WATASHANGILIWA NA MASHABIKI 447 TU, MOTO UTAWASHWA KESHO YAKE.


Wanaume wa kazi kesho wanavaana na Barcelona

Mashabiki wa Atletico Madrid watashangilia ubingwa wa La liga kwa saa 48 kama watatwaa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 18


KAMA Barcelona watashinda kesho dhidi ya Atletico Madrid na kutwaa taji la La Liga, siku inayofuata hawatakuwa na sherehe ya kushangilia ubingwa ndani ya basi lao la wazi na kupita  mitaa ya Barcelona.
Hii inatokana na kushindwa kuonesha makali msimu huu, hivyo wanaona hakuna haja ya kufurahia mafanikio kiduchu namna hiyo.

Wachezaji, makocha, wakurugenzi na mashabiki wa Barca walishakata tamaa ya kutwaa ubingwa siku nyingi, kwahiyo kama watashinda kesho na kutwaa ubingwa wataondoka uwanjani ndani ya muda mfupi.
Wachezaji wa klabu hiyo wataondoka siku ya kesho yake na kwenda kujiunga na timu zao za taifa kujiwinda na michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

LA LIGA: PAZIA KUFUNGWA KESHO

Siku ya mwisho kesho wapenzi wa soka watashuhudia Barcelona na Atletico wakichuana kwa mara ya tatu katika historia yao.

Barcelona wataweza kushinda taji kutokana na rekodi nzuri ya `head-to-head`  kama watawafunga Atletico Madrid.

Sare itatoshwa kuwapa Atletico ubingwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 18.

HEAD-TO-HEAD
21 August: Atletico 1-1 Barcelona
(Spanish Super Cup)
28 August: Barcelona 0-0 Atletico
(Spanish Super Cup)
11 January: Atletico 0-0 Barcelona
(La Liga)
1 April: Barcelona 1-1 Atletico
(Champions League)
9 April: Atletico 1-0 Barcelona
(Champions League)

Kama Atletico Madrid watashinda taji kesho hakuna atakayelala ndani ya saa 48 ndani ya mji mkuu wa Hispania.

Mshabiki 447 ndio waliopata tiketi za kushabikia timu ya Atletico hapo kesho, lakini kama watashinda, moto utawashwa tena mapema jumapili nyumbani kwao Madrid.

Timu hizi mbili zitashangilia ubingwa kwa staili tofauti kabisa. Wakatalunya watamfuta kazi Kocha mkuu, Tata Maryino bila kujali  kitakachotokea kesho jumamosi.

Mlinda mlango Victor Valdes atajiunga na Monaco. Dani Alves  atamfuata nchini Ufaransa kwa kujiunga na PSG. Beki Carles Puyol atajiunga na kocha mpya anayekuja, Luis Enrique kwenye benchi la ufundi.

Alex Song, Javier Mascherano, Pedro na Alexis Sanchez wote wanauzwa na wanaweza kuondoka kama ofa nzuri zitapatikana, huku Barcelona wakijiandaa kumsajili beki wa Chelsea, David Luiz.

Barca wanaweza kuwashawishi Chelsea kwa kuwapatia Alex Song na Alexis ili kuinasa saini ya Luiz.

0 Responses to “BARCELONA HAWATASHEREHEKEA UBINGWA WA LA LIGA.....NAO ATLETICO WATASHANGILIWA NA MASHABIKI 447 TU, MOTO UTAWASHWA KESHO YAKE.”

Post a Comment

More to Read