Mkazi wa
Mtaa wa King’azi, Mbezi Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam (jina tunalihifadhi),
amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo kukatwa sehemu za
siri na mumewe kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Mwanamke
huyo alikumbwa na adha hiyo juzi saa nne usiku nyumbani kwake na hadi jana, saa
nne asubuhi baadhi ya vipande vya nyama vya sehemu za siri na chini ya tumbo,
jirani na kitovu, vilikuwa bado vipo katika eneo la tukio.
Ofisa
Habari wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Gerald Chami alisema jana kwamba kutokana
na majeraha aliyokuwa nayo alipelekwa katika chumba cha upasuaji kushonwa.
Chami
alisema majeruhi huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa tabu alisimulia kwamba
siku moja kabla ya tukio, mumewe alimkuta akiongea na simu ya mkononi na
alimnyang’anya na kuisikiliza na alipobaini kuwa ni sauti ya mwanamume
hakuuliza kitu, bali alimrudishia simu na kuondoka.
Alisema
muda mfupi baadaye alirudi akionyesha dalili za kuwa na hasira na ndipo mama
huyo alipomhoji mumewe juu ya hatua yake ya kumnyang’anya simu na kumuuliza
ilikuwa na shida gani. Hatua hiyo ilisababisha ugomvi mkubwa.
Chami
alisema mwanamke huyo alimwambia kuwa baada ya ugomvi huo, aliamua kuondoka
nyumbani hapo na kwenda kwa ndugu yake jirani lakini muda mfupi baadaye, mume
wake alimfuata na kumlazimisha kurudi nyumbani lakini alimkatalia na kumtaka
wazungumze ugomvi wao hapohapo ili wapate suluhu.
“Huyu mama
alisema katika ubishi huo wa wapi wakajadili ugomvi wao huo, ndipo ndugu zake
wakamshauri kuwa kwa vile mumewe alitaka wakayamalize kwao basi aende.
Hata
hivyo, walipofika nyumbani badala ya kujadili ugomvi, alianzisha tena ugomvi na
kisha kuchukua kisu na kumtishia kumchinja na katika patashika hiyo, Chami
alisema mama huyo alimweleza kwamba aliishiwa nguvu na kuanguka ndipo mwanamume
huyo alipomjeruhi vibaya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema licha ya kwamba mgonjwa huyo huko
Tumbi, asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa lilitokea katika Mkoa wa
Kipolisi wa Kinondoni.
0 Responses to “MWANAMKE AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI KWA KISU NA MMEWE BAADA YA KUMKUTA AKIONGEA KWA SIMU NA MWANAMME MWINGINE ”
Post a Comment